sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Dunia

Fahamu namna ya kuisadia dunia kuwa na chakula cha kutosha kufikia 2030

media Chakula maarufu sana Afrika Mashariki na Kati, Ugali, nyama na mboga za majani www.trainingarunner.com

Umoja wa Mataifa unalenga kuwa, kufikia mwaka 2030, uwe umemaliza baa la njaa duniani.

Kila tarehe 16, Umoja huo hutumia siku hiyo kuhimiza umuhimu wa dunia isiyo na njaa na kuangalia mbinu za kufikia malengo hayo.

Unaweza kufanya nini ili kuwa na dunia isiyikuwa na njaa ?

Epuka matumizi mabaya ya chakula

Iwapo kuna chakula kimebaki, kihifadhi kwa matumizi ya baadaye, usikimwage. Unapokula Mkahawani au hotelini, agiza chakula unachoweza kukimaliza na kikibaki, kibebe uende nacho nyumbani.

Zalisha chakula zaidi

Idadi ya watu duniani inapotarajiwa kukua na kufikia Bilioni 9 kufikia mwaka 2050, wakulima wanastahili kutafuta mbinu  za kisasa  kuzalisha chakula zaidi. Mbinu hizo zitawasadia Wakulima kuzalisha chakula zaidi na kuwasaidia kupata faida.

Kula mlo kamili

Pata mbinu za kupika na kupata mlo kamili, utakaokufanya kuwa na afya njema. Unaweza kupika chakula kama hiki kwa kutumia viungo rahisi. Aidha, unaweza kuwasiliana na Mkulima kuona namna anavyopika chakula chake nyumbani kwake.

Harakati za kampeni

Kila mmoja ana jukumu la kutoa elimu kuhakikisha kuwa, dunia inafahamu umuhimu wa kuwepo kwa chakula na madhara ya njaa. Kufanikiwa katika hili ni muhimu viongozi wa eneo unalohisi na wale wa kitaifa kuhusishwa kikamilifu.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana