Pata taarifa kuu
WAISLAMU-EID AL FITR-DINI

Waislamu waadhimisha sikukuu ya Eid al fitr

Waislamu kutoka Afrika Mashariki na Kati wanaungana na wenzao dunia, kusherehekea sikukuu ya Eid al fitr siku ya Ijumaa. 

Eid al Fitr kwa Waislamu wote duniani
Eid al Fitr kwa Waislamu wote duniani wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Hii ni siku ambayo Waislamu wanashiriki katika sala la pamoja baada ya kumaliza kipindi cha mwezi mmoja wa mfungo wa Ramadhan.

Mbali na kufanyika kwa sala misikitini na maeneo mengine ya wazi, ni siku ya Waislamu kukutana na wapendwa wao na kula pamoja lakini pia kuwasaidia wale ambao wana uhitaji katika jamii.

Historia ya siku hii:

Katika Dini ya Kiislamu, Eid ni sherehe ya muhimu sana , na inaonyesha Upendo, kusherehekea maisha, na uaminifu kwa Mungu Allah.

Sherehe mbili za eid kwa mwaka kwa waislamu ni Eid ul fitrna Eid ul Adha.

Eid maana yake ni Sherehe, inajulikana yenyewe, Mubarak maana yake ni Baraka.

Wakati wa Eid ul fitr watu husalimiana kila mmoja  kwa neno la Baraka ambalo ni Eid Mubarak.

Eid Ul fitr ilianzishwa na Mtume Muhammad.Inaanzia mwenzi wa kwanza wa Shawwal na mwisho wa mwezi wa  Ramadhan, Wakati ambao waislamu wako kwenye kipindi cha mfungo.

Eid Mubarak kwa Waislamu wote duniani kutoka hapa RFI Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.