Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-SILAHA ZA KEMIKALI

Uchunguzi wa kimataifa kufanyika kuhusu mashambulizi ya kemikali Syria

Mkutano wa Shirika la kimataifa linalopiga marufuku matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) umepangwa kufanyika leo Jumatatu, siku moja baada ya uzinduzi wa uchunguzi wa wataalam wake kuhusu madai ya mashambulizi ya kemikali nchini Syria.

Mji wa Douma uliodaiwa kushambuliwa kwa silaha za kemikali
Mji wa Douma uliodaiwa kushambuliwa kwa silaha za kemikali fr.news.yahoo.com
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalisababisha mashambulizi ya nchi za Magharibi dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad na kusababisha kuongezeka kwa kasi kwa mvutano wa kidiplomasia.

Siri kubwa imetanda kwa kazi ya ujumbe wa Shirika la kimataifa linalopiga marufuku silaha za kemikali (OPCW), ambalo lina mamlaka ya kuchunguza uwezekano wa matumizi ya silaha za kemikali lakini si kwa kutambua wahusika.

Maelezo machache yametolewa kuhusu mkutano uliopangwa kufanyika kwenye makao makuu ya OPCW huko The Hague.

Siku ya Jumapili, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Fayçal Mokdad, alitembelea hoteli moja ambako ujumbe wa OPCW umepiga kambi mjini Damascus na aliondoka saa tatu baadaye, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Ujumbe wa uchunguzi wa OPCW unatarajia kuanza kazi yake kwa mfululizo wa mahojiano ya kibinafsi na viongozi wa Syria.

Kwa upande mwingine, haijathibitishwa kuwa wataalam hao watatembelea mji wa Douma, kama afisa mmoja wa serikali ya Syria alivyoliambia shirika la habari la AFP.

"Tutaacha timu ya wataalam hao kufanya kazi kwa ustadi, kwa usahihi, bila ya upendeleo na mbali na shinikizo lolote. Matokeo ya uchunguzi yatabainisha madai ya uwongo" dhidi ya serikali ya Damascus, amesisitiza afisa huyo wa Syria.

Wakati huo huo Rais wa Urusi Vladimir Putin, mshirika mkubwa wa Syria, alionya siku ya Jumapili Marekani, Ufaransa na Uingereza, nchi tatu ambazo ziliendesha operesheni ya kijeshi: "mashambulizi mapya yatasababisha "machafuko" katika mahusiano ya kimataifa, alisema, akinukuliwa katika taarifa ya Kremlin iliyotolewa baada ya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Iran Hassan Rohani, mshirika mwingine mkubwa wa serikali ya Syria.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley ametangaza kuwa leo Jumatatu Marekani itaweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuhusiana na matumizi ya silaha za kemikali na serikali ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.