Pata taarifa kuu
UINGEREZA-ELIMU-SAYANSI

Msomi maarufu wa Fizikia duniani Profesa Stephen Hawking afariki dunia

Mwanafizikia maarufu duniani raia wa Uingereza Profesa Stephen Hawking, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Profesa Stephen Hawking, wakati wa uhai wake
Profesa Stephen Hawking, wakati wa uhai wake REUTERS/Neil Hall
Matangazo ya kibiashara

Familia yake imethibitisha kifo chake na atakumbukwa sana katika kipaji chake cha kipekee katika tasnia ya Sayansi licha ya kuwa na ulemavu, uliomfanya kutumia kiti cha magurudumu katika kipindi chote cha maisha yake.

Mwaka 1988 aliandika kitabu kilichopewa jina "A Brief History of Time" kilichojaribu kuelezea hali ya dunia na angani.

Atakumbukwa kama Mwanasayansi wa kipekee ambaye licha ya ulemavu wake, haukumzuia kutoa mchango wake katika kuimarika kwa sekta hiyo.

Ameishi miaka 76, licha ya Madaktari kusema kuwa angeishi kwa muda wa miaka miwili tu baada ya kupata ugonjwa nadra sana mwaka 1964 akiwa na umri wa miaka 22 na kumsababishia ulemavu.

Hakuweza kuongea kawaida, lakini alitumia kifaa maalum kilichomsaidia kuwasiliana.

Mwaka 1979, aliteuliwa kuwa Mhadhiri wa somo la Hesabu katika Chuo Kikuu cha Cambridge.

Alipata elimu yake kutoka chuo kikuu cha Oxford.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.