Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-KOMBE LA DUNIA URUSI 2018

FIFA yatangaza droo ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi

Shirikisho la soka duniani FIFA, limetangaza droo ya michuano ya kombe la dunia litakalofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Droo ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi
Droo ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi Alexander NEMENOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika sherehe za kufana zilizofanyika jijini Moscow siku ya Ijumaa jioni, na kuhudhuriwa na rais wa Urusi Vladimir Putin, rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino ni miongoni mwa wageni mashuhuri na wachezaji wa zamani waliohudhiria michuano hiyo.

Rais Putin amesema nchi yake iko tayari kuandaa michuano hiyo ambayo amesema itasaidia kuimarisha mchezo wa soka nchini humo na kwingineko duniani.

Mataifa 32 yatakayoshiriki katika michuano hiyo, yamepangwa katika makundi manane, kila kundi likiwa na timu nne.

Michuano hiyo itachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 kati ya tarehe 14 mwezi Juni hadi tarehe 15 mwezi Julai mwaka 2018.

Bara la Afrika litawakilishwa na Nigeria, Misri, Senegal, Tunisia na Morocco.

Hii ndio droo kamili:-

Kundi  A: Urusi (Wenyeji), Saudi Arabia, Misri, Uruguay.

Kundi B: Ureno, Uhispania, Morocco, Iran.

Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark.

Kundi  D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria.

Kundi  E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia.

Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden, Korea Kusini.

Kundi G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, Uingereza.

Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.