UNHCR: Idadi ya wakimbizi yaongezeka na kufikia Milioni 65.6 duniani
Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya wakimbizi duniani imeongezeka na kufikia Milioni 65.6 .
Imechapishwa: Imehaririwa:
Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi inasema hili ni ongezeko la wakimbizi 300,000 ongezeko lililoshuhudiwa mwaka 2016.
Mkuu wa Tume hiyo Filippo Grandi amesema inasikitisha kuona idadi ya wakimbizi ikiendelea kuongezeka duniani kila wakati.
“Dunia inaonekana kushindwa kulinda amani,” amesema Bwana Grandi.
Soma pia makala haya:-Bonyeza
Aidha, amesema asilimia 84 ya wakimbizi hao wanaishi katika mazingira magumu na ya umaskini.
Maeneo yaliyo na wakimbizi wengi ni kutoka barani Afrika, Mashariki ya Kati na barani Asia.
Nchi wanazotokea idadi kubwa ya wakimbizi:
- Syria: Zaidi ya Milioni 5.5
- Afghanistan: Milioni 2.5
- Sudan Kusini: Milioni 1.4
Mataifa yepi yanaongoza kuwapa hifadhi wakimbizi ?
- Uturuki : Milioni 2.9
- Pakistan: Milioni 1.4
- Lebanon: Milioni 1
- Iran: 979,4000
- Uganda: 940,800
- Ethiopia: 791,600