Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-KENYA

Mwanasiasa mwenye asili ya Kenya akaribia kuwa Seneta nchini Australia

Mwanasiasa mwenye asili ya Kenya Lucy Gichuhi anatarajiwa kuwa Mwafrika wa kwanza kuingia katika bunge la Senate nchini Australia.

Lucy Gichuhi mwanasiasa wa Australai mwenye asili ya Kenya
Lucy Gichuhi mwanasiasa wa Australai mwenye asili ya Kenya Yutube
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama kuthibitisha kuwa alishinda Uchaguzi baada ya kura kuhesabiwa upya.

Anachosubiri kwa sasa ni uamuzi rasmi wa Mahakama ili kuungana na bunge hilo la Maseneta 76.

Vyombo vya Habari nchini Australia vinaripoti kuwa Bi.Gichuhi aliye na uraia  wa nchi hiyo anatarjiwa Mwafrika wa kwanza kutokea nchini Kenya kuwa Seneta.

Mwanasiasa huyo aliondoka nchini Kenya mwaka 1999 na kuamua kuchukua uraia wa Australia.

Baada ya kuingia katika ulingo wa kisiasa, aliamua kuachana na uraia wa Kenya lakini kumekuwa na utata ikiwa kweli ameachana na uraia wa nchi yake ya zamani.

Mahakama sasa inasubiriwa kufanya uamuzi wake wa mwisho.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.