Pata taarifa kuu
URUSI - USALAMA

Mshambuliajii wa Saint Petersbourg atambulika

Wakati uchunguzi ukiendelea kumbaini muhusika wa tukio la shambulio la Saint Petersbourg nchini Urusi, rais wa nchi hiyo Vladimir Poutine ameweka jana jioni shahada la maua katika ene la tukio la shambulizi hilo lililogharimu maisha ya watu 11. Kwa mujibu wa ripota wa RFI aliepo huko Moscou Etienne Bouche, shambulio hilo lina kila dalili za tukio la kigaidi.   

Rais Vladimir Poutine amejielekeza katika kituo cha Tekhnologichesky, jana jioni, avril 3,  2017.
Rais Vladimir Poutine amejielekeza katika kituo cha Tekhnologichesky, jana jioni, avril 3, 2017. REUTERS/Grigory Duko
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa duru zilizotajwa na kituo cha habari cha Urusi, ni shambulio la kujitoa muhanga. mshambuliaji anaelezwakuwa kijana aliebeba bomu kwenye begi la mgongoni, ambapo taarifa zaidi zinaeleza kwamba vilipuzi hivyo vinafana na vilivyogundulika katika kituo kimoja cha treni mjini kati.

wakati hayo yakiarifiwa Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa nchi yake itatoa msaada wa hali na mali kwa serikali ya Urusi wakati huu ikikabiliana na athari za shambulio lililotokea katika kituo cha treni za mwendo kasi mjini Saint Petersburg.

Rais Trump amelezea kusikitishwa kwake na kulaani shambulio hilo lililosababisha watu wasiopungua 11 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa na serikali ya Urusi inaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo linalodhaniwa kuwa la kigaidi.

Trump amezungumza kwa simu na rais wa Urusi Vladimir Putin na kumweleza kuwa Marekani itasaidiana na Urusi kukabiliana na shambulio hilo na kuhakikisha wahusika wanafikishwa mbele ya vyombo sheria ili haki itendeke.

Kwa pamoja rais Donald Trump na rais Vladimir Putin wamekubaliana kuwa vitendo vya kigaidi havikubaliki kwa sasa na lazima nguvu za pamoja zitumike kupambana navyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.