Pata taarifa kuu
JAPAN-G7-UCHUMI

Mkutano wa G7 kuzungumzia uchumi duniani, ugaidi, uhamiaji

Viongozi kutoka nchi zilizoendelea kiviwanda (G7), waanza Alhamisi hii mkutano wa kilele nchini Japan kwa ajenda kubwa kati ya changamoto za ukuaji dhaifu wa kimataifa, mapambano dhidi ya ugaidi, madai ya China kuhusu umiliki wa eneo moja la bahari au uhamiaji.

Wakuu wa nchi au serikali kutoka Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani, Canada na Japan wanakutana katika mji wa Ise-Shima, Japan.
Wakuu wa nchi au serikali kutoka Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani, Canada na Japan wanakutana katika mji wa Ise-Shima, Japan. STEPHANE DE SAKUTIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi au serikali kutoka Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani, Canada na Japan wanakutana katika mji wa Ise-Shima, mkoa wa pwani uliyo katika milima yenye miti, katikati mwa Japan.

Kabla ya kuingia mazungumzo magumu ambayo yatafuatiwa siku ya Ijumaa na ziara ya kihistoria ya Barack Obama katika mji wa Hiroshima, mji uliyoshambuliwa na Marekani kwa silaha za nyuklia mwaka 1945. Viongozi wa G7 wametembelea kaburi la Ise-Jingu, sehemu takatifu kwa raia wa Japan.

Siku chache tu baada ya mkutano wa Mawaziri wa Fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi hizi saba katika mji wa Sendai (kaskazini- mashariki), udhaifu wa ukuaji wa kimataifa utaibua maswali mengi katika mazungumzo ya viongozi hao kutoka nchi saba zilizoendelea kiviwanda.

"Uchumi wa dunia utapewa kipao mbele katika mkutano wa kilele wa G7 katika mji wa Ise-Shima," Bw Abe alisema Jumatano wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Obama. "Rais Obama na mimi tunatambua kwamba G7 inapaswa kutafuta ukuaji wa jumla, endelevu na imara".

Usalama umeimarishwa katika mji wa Ise-Jingu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.