Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-UGAIDI

Ufaransa yaisihi Ubelgiji kuwatuma washukiwa 4

Ufaransa inaitaka Ubelgiji kuwasafirisha washukiwa wanne wa ugaidi, wanaotuhumiwa kutekeleza shambulizi la kigaidi jijini Paris mwaka uliopita.

Askari polisi katika mji wa Molenbeek, ambapo Abdeslam Salah alikamatwa Ijumaa, Machi 18, 2016.
Askari polisi katika mji wa Molenbeek, ambapo Abdeslam Salah alikamatwa Ijumaa, Machi 18, 2016. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa watatu kati ya hao wanne wanatuhumiwa kumsadia mshukiwa mkui Salah Abdeslam, kutoroka nchini Ufaransa baada ya mashambulizi hayo.

Abdeslam alikamatwa mwezi Machi na amekuwa akihojiwa kuhusu mashmabulizi ya jiji la Paris na yale yaliyotokea katika uwanja wa ndege jijini Brussels mwezi Machi mwaka huu.

Kama watuhumiwa watakubaliana na jambo hilo la kusafirishwa Ufaransa, zoezi hilo linapaswa kufanyika ndani ya siku kumi.

Wanasheria wa watuhumiwa watatu kati ya wanne wamethibitisha kwamba wateja wao wako tayari kusafirishwa Ufaransa. Watuhumiwa Hamza Attou na Mohamed Amri waliitwa na Salah Abdeslam akiwa mjini Paris baada ya mashambulizi ya jioni Novemba 13 na waalikuja mjini Brussels kumtafuta.

Mtuhumiwa mwengine watatu anayeombwa na mahakama ya Ufaransa ni Ali Oulkadi, ambaye alimsafirisha kwa gari Salah Abdeslam hadi mafichoni katika ghorofa ambapo alama zake za vidole ziligunduliwa mwezi Desemba.

Jina la mtuhumiwa mwengine wanne anayeombwa na mhakama ya Ufaransa halijajulikana. Lakini huenda ni MohamedBakkali, ambaye alikodi gari na kuwasafirisha washambuliaji kabla ya mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.