Pata taarifa kuu
UFARANSA-PALESTINA-ISRAEL

Ufaransa mwenyeji wa mazungmo kati ya Israel na Palestina

Ufaransa imetangaza kuwa itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa kujadili mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati hasa kati ya Palestina na Israel.

Mkutano kati ya Benjamin Netanyahu na Mahmoud Abbas ulifanyika Julai 29, 2013 jioni Washington, Marekani.
Mkutano kati ya Benjamin Netanyahu na Mahmoud Abbas ulifanyika Julai 29, 2013 jioni Washington, Marekani. Reuters/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje nchini humo inasema lengo la mkutano huo ni kurejesha mazungumzo hayo ya amani ili kujaribu kupata mwafaka wa kudumu.

Mkutano huo umepangwa kufanyika tarehe 3 mwezi ujao, na tayari Palestina imekubali kushiriki lakini Isreal inasema haitaki mkutano wa kimataufa bali inataka mazungumzo ya moja kwa moja na Palestina.

Misri imekuwa ikisema kuwa iko tayari kuwa mpatanishi katika mazungumzo hayo ili kusaidia pande hizo mbili kupata mwafaka.

Juhudi za Marekani katika miaka iliyopita kusaidia Palestina na Israel kupata amani ya kudumu hazijafanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.