Pata taarifa kuu
MAREKANI-UGANDA-BASHIR

Marekani yalaani Uganda kumwalika Bashir

Marekani imemshtumu rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kumwalika rais wa Sudan Omar Al Bashir katika sherehe za kumwapisha hapo jana jijini Kampala.

Rais Yoweri Museveni wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa muhula wa tano mbele ya Marais mbalimbali wa kigeni, ikiwa ni pamoja na Rais wa Sudan Omar el-Bashir, Mei 12, 2016.
Rais Yoweri Museveni wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa muhula wa tano mbele ya Marais mbalimbali wa kigeni, ikiwa ni pamoja na Rais wa Sudan Omar el-Bashir, Mei 12, 2016. © RONALD KABUUBI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Bashir anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa tuhma za kuhusika na mauaji ya maelfu ya watu katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Matamshi ya rais Museveni hapo jana kuhusu ICC, yamewakera viongozi wa nchi za Magharibi na Mabalozi kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Canada waliondoka katika sherehe za kumwapisha rais Museveni baada ya rais huyo kusema kuwa Mahakama ya ICC haina maana.

Maelfu ya raia wa Uganda, wakiwemo viongozi kadhaa wa bara la Afrika wameshuhudia kuapiashwa kwa rais Yoweri Kaguta Museveni kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo.

Akiwahotubia maelfu ya raia wa Uganda na wageni wengine mashuhuri katika uwanja wa Kololo jijini Kampala, Rais Museveni amesema, katika uongozi wake wa miaka mitano ijayo, atahakikisha kuwa Uganda inakuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

Kuhusu usalama, rais Museveni amesema nchi yake kwa muda wa miaka 30 alizokuwa madarakani ina amani ya kutosha ndani ya miaka 500 ya historia ya nchi hiyo, na kutoa wito kwa mataifa ya Afrika kusaidia nchi zingine kupata amani kama hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.