Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Taliban yatangaza kuanza vita Afghanistan

Wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan, ambao nchi nyingi zinajaribu kuwashawishi kukaa katika meza ya mazungumzo na serikali ya Kabul, Jumanne hii, wametangaza kuanza "vita vyao vya majira ya kiangazi".

Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35%  ya nchi ya Afghanistan.
Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35% ya nchi ya Afghanistan. AFP PHOTO / Noorullah Shirzada
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wamesema katika taarifa waliotoa nia yao ya "kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya ngome za maadui nchini kote." Wameyaita mashambulizi hayo kwa jina la "Operesheni Omari" kwa heshima ya Mullah Omar, mwanzilishi wa kundi la Taliban ambaye kifo chake kilitangazwa katika majira ya joto mawaka jana.

Mashambulizi ya majira ya baridi ya kundi la taliban yanatoa nafasi ya "msimu wa mapigano" nchini Afghanistan baada ya mapumziko katika majira ya baridi. Lakini katika majira haya ya baridi, mapigano yaliendelea nchini kote.

Wapiganaji wa Taliban wametangaza operesheni "zilizoendeshwa na mashujaa dhidi ya ngome za maadui" ikimaanisha, mashambulizi ya kujitoa mhanga, mbinu ambayo mara nyingi hutumia, kwa kawaida dhidi ya polisi na jeshi la Afghanistan ambao inawachukulia kama kama "watumwa" wa askari wa kigeni waliotumnwa nchini Afghanistan. Jumatatu hii, wanajeshi wapya 12 waliuawa katika shambulio la kujitoa mhanga lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban mashariki mwa nchi hiyo.

Lakini wapiganaji wa taliban, ambao wanaendesha mashambulizi tangu kuanguka kwa utawala wao mwaka 2001, pia wanapanga kuwashambulia askari 13,000 wa Umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ili "kuwakatisha tamaa na kuwalazimisha kuondoka nchini mwao". hayo waliyasema katika taarifa yao waliyoitumwa katika ofisi ya vyombo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi ya shirika la habari la Ufaransa la AFP. vile vile taarifa hii imerushwa kwenye Intaneti.

Kuondoka kwa askari wa kigeni ni moja ya masharti makua ya wapiganaji wa Taliban ili waweze kurudi katika meza ya mazungumzo.

Majira yaliyopita, mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja yalifanyika nchini Pakistan. Lakini yalivunjika ghafla baada ya kutangazwa kifo cha Mullah Omar.

Kwa kujaribu kufufua mchakato huu wa amani wa moja kwa moja, Afghanistan, Pakistan, China na Marekani wanakutana mara kwa mara mjini Islamabad na Kabul tangu mwezi Januari. Juhudi hizi bado hajazaa chochote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.