Pata taarifa kuu
CANADA-SYRIA

Canada kusitisha mashambulizi nchini Syria

Serikali ya Canada imetangaza kuwa, inasitisha mashambulizi ya anga yanayolenga wapiganaji wa kijihadi wa Islamic State nchini Iraq na Syria ikiwa ni pamoja na kuzirudisha nyumbani ndege zake 6 za kivita ifikapo February 22, amesema waziri mkuu Justin Trudeau akitekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.

waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini  Ottawa, akitangaza kusitisha mashambulizi ya anga nchini Syria Februari 8, 2016.
waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini Ottawa, akitangaza kusitisha mashambulizi ya anga nchini Syria Februari 8, 2016. REUTERS/Chris Wattie
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wake na vyombo vya habari Justin Trudeau ametetea mabadiliko yake ya siasa za mashariki ya kati na kupendelea kuweka mbele msaada wa moja kwa moja na wa muhimu badala ya ndege sita za kivita.

Trudeau amesisitiza kuwa mashambulizi ya anga ni muhimu kweli kushinda kwa muda mfupi kijeshi kwenye uwanja wa mapambano, lakini hayaleti utulivu wa kudumu kwa raia, huku akitowa mfano wa Afghanistan ambako Canada ilikuwa na nafasi kubwa katika kutoa mafunzo ya kijeshi kwa viksoi vya ulinzi nchini Afghanistan.

waziri mkuu huyo ameendelea kuwa wananchi wanaotiwa hofu kila siku na kundi linalojiita Islamic State, hawana shida ya ulipizaji wetu kisase, bali wanayo shida ya msaada wa moja kwa moja kutoka kwetu.

Licha ya hivo Canada imesema itazidisha idadi ya wanajeshi wake maalum wanaotoa mafunzo ya kijeshi nchini iraq ambapo hadi mwezi Septemba mwaka 2014 walikuwa wanajeshi 70 eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, huku wanajeshi 600wakitumwa kusaidia katika mashambulizi ya anga.

Hata hivyo kuna mgawanyiko mkubwa wa kimtazamo kuhusu uamuzi wa waziri mkuu, huku tangazo lake likienda kinyume na maoni ya wananchi wengi wa Canada ambao wanaunga mkono operesheni za mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State.

Waziri mkuu Justin Trudeau, anasema kuna watu watakosoa hatua yake lakini wacha iwe hivyo, kwakuwa operesheni za kijeshi zina majibu ya muda mfupi kuliko suluhu ya kudumu.

Wachambuzi wa mambo nao wanaona kuwa uamuzi wa Canada unaweza kuwa na faida pamoja na hasara kwa upande wao, sababu utatoa mwanya kwa wpaiganaji wa Islamic state kulipiza kisasi na kwa upande mwingine kuzuia mashambulizi hayo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.