Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA

Davotuglu: Uturuki haiwezi kubeba pekeake mzigo wa wahamiaji

Waziri mkuu wa Uturuku Ahmet Davutoglu amesema takriban wakimbizi 30.000 wamekusanyika karibu na mpaka na Uturuki baada ya vikosi vya serikali ya Damascus kuanzishwa operesheni katika mji wa Allep. Waziri Davutoglu ameyasema hayo mbele ya vyombo vya habari jijini Ankara wakati wa ziara ya Kansela WA ujerumani Kansela Angela Merkel nchini Utruruki.

waziri mkuu nchini Uturuki, Ahmed Davutoglu
waziri mkuu nchini Uturuki, Ahmed Davutoglu REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Akizungungumza na waandishi wa habari jijini Ankara Ahemd Davutoglu amesema nchi yake haiwezi kuvumilia yao pekeake mzigo wa kuwapokea wakimbizi wa Syria wakati huu kukiwa na wimbi jingine jipya la wakimbizi wanaokimbia mapigano ya hivi karibuni katika mji wa Allepo na kukusanyika katika eneo la mpaka wa Uturuki na Syria.

Davutoglu amesisitiza kuwa sio kwamba Uturuki imekubali kuwpaokea wakimbizi itachukuwa majukumu yote pekeake na kubeba mzigo wote wa mapokezi.

Hayo yanajiri wakati huu watu 35 wanaodaiwa kuwa wakimbizi wakiarifiwa kupoteza maisha leo Jumatatu katika ajali iliotokea kwenye bahari ya Egee karibu na ufukwe wa Uturuki wakati wakijaribu kuingia katika kisiwa kisiwa kimoja nchini Uturuki.

Ajali hiyo imetokea katika matukio mawili tofauti katika ufukwe wa mji wa Dikili mkoa wa Izmir magharibi ambako wakimbizi walikuwa wakielekea katika eneo la Lesbos na kusababisha 11 kupoteza maisha. Wahudumu wawili katika meli hiyo wameokolewa na walinzi wa upande wa Uturuki.

Ajali nyingine ilitokea wakati wahamiaji wengine 24 walipokuwa wakijaribu kuelekea katika eneo la Lesbos na kufa maji baada ya chombo walichokuwa wakisafiria kuzama katika eneo la Edremit magharibi kaskazini mwa jimbo la Dikili. Watu 4 wameokolewa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.