Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-Mapigano-Usalama

Mashambulizi ya Uturuki dhidi ya waasi wa PKK yaendelea

Mji wa Kobane unaendelea kukabiliwa na mapigano, na huenda hali hiyo ikasababisha mchakato wa amani kati ya waasi wa PKK na serikali ya Uturuki unaingia matatani.

Wakurdi wanaagalia mapigano yanayoendelea katika mji wa Kobane, nchini Syria.
Wakurdi wanaagalia mapigano yanayoendelea katika mji wa Kobane, nchini Syria. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumatatu jioni wiki hii jeshi la Uturuki linaendelea kushambulia ngome za waasi wa PKK nchini Uturuki.

Serikali ya Uturuki inawaatuhumu waasi wa PKK kuanzisha mapigano, lakini wakaazi wa mji mkuu wa Wakurdi, Diyarbakir, wanaona kwamba viongozi wa Uturuki wameamua kuvunja mchakato wa amani.

Hata hivo maandamano yaliokua yameandaliwa jana jumanne kuunga mkono mji wa Wakurdi wa Syria na kupinga machafuko yanayoendelea katika mji wa Kobane, yamegeuzwa muelekeko na kuwa maandamano ya kuunga mkono chama cha PKK, wakati ambapo tawi la kijeshi la chama hicho limekua likilengwa na mashambulizi anga ya jeshi la Uturuki tangu Jumatatu jioni wiki hii.

“ Lengo la seriklai ya Uturuki ni kuvunja chama cha PKK na watu kutioka jamii ya Wakurdi. Sote hapa tunaunga mkono chama cha PKK. Raia wa Uturuki wanafikiri kwamba wataishi kwa amani, wanajidanganya. Tutafanya kinacho hitajika ili wakubali matakwa yetu !”, mmoja kati ya vijana wa Kikurdi amethibitisha.

“ Mimi nina imani kwamba mchakato wa amani haujavunjwa, licha ya Uturuki kuanza mashambulizi hayo. Inabidi pande mbili husika kuketi pamoja ili kuendeleza mchakato huo. Na iwapo Uturuki imeazimia kuanzisha vita dhidi ya PKK, hakuna tutakacho badili, lakini nina imani kwamba hali hiyo haiwezi ikatokea”, amesema mmoja kati ya waandamanaji.

Wakurdi wamekua wakiinyoshea Uturuki kidole cha lawama kwamba haina nia yoyote ya kufanya machambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, ambao wanaendelea kuteka baadhi ya maeneo ya mji wa Kobane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.