Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Dunia

Malala Yousafzai na Kailash Satyarthi watunukiwa tuzo ya amani ya Nobel

media Watanaiwa wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2014: Kailash Satyarthi, raia wa India mwenye umri wa miaka 60 (kushoto), Malala Yousafzaï, msichana wa Pakistan mwenye amri wa miaka 17 (kulia). REUTERS/Adnan Abidi/Carlo Allegri/Files

Malala Yousafzaï msichana wa Pakistan pamoja na Kailash Satyarthi kutoka India wametunikiwa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na jitihada zao za kuhamasisha na kupambana juu ya elimu kwa watoto, kamati iliyotoa tuzo hiyo imebaini.

Malala Yousafzaï, mwenye umri ya miaka 17 ni mtaniwa wa kwanza kijana kutunukiwa tuzo hiyo ya amani ya Nobel. Anachukua nafasi ya Lawrence Bragg, raia wa Uingereza mwenye asili ya Australia aliye tunukiwa tuzo ya Fizikia ya Nobel pamoja na baba yake akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 1915.

Ni sharti muhimu kwa maendeleo ya dunia iwapo haki za watoto zitazingatiwa”, imeeleza kamati iliyotoa tuzo hiyo ya amani ya Nobel.

Malala Yousafzaï alizaliwa katika kijiji cha Mingora eneo la Swat nchini Pakistan, lakini alikabiliwa na misukosuko mingi baada ya kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wasichana kwenda shule.

Malala Yousafzaï alianzisha kampeni hiyokupitia blog ya idhaa ya Ourdu ya BBC ambapo alikua akihamasisha wasichana kwenda shule. Harakati hizo alizianza akiwa na umri wa miaka 11, harakati ambazo zilipingwa na makundi ya wapiganaji wa kiislam. Malala alinusurika kifo wakati alipopigwa risase kichwani na wapnaji wa Taliban Oktoba mwaka 2012.

Wakati huu Msichana huyo anaishi nchini Uingereza, ambapo alifanyiwa matibabu hadi kupona. Malala Yousafzaï alianzisha kampeni inayojulikana kwa jina lake kwa niaba ya watoto katika nchi mbalimbali, hususan Pakistan, Nigeria, Jordan, Syria na Kenyas

Kwa upande wake Kailash Satyarthi, mwenye umri wa miaka 60, ambaye pia ametunikiwa tuzo ya amani ya Nobel, anafuata nadharia ya Ghandi, kulingana na uamzi wa kamati iliyotoa tuzo hiyo, ikikumbusha kwamba raia huyo wa India aliongoza maandamano mbalimbali ya amani yenye lengo la kutafuta mageuzi dhidi ya kutumiwa kwa watoto kwa maslahi ya kifedha.

Tuzo hiyo itakabidhiwa rasmi kwa wataniwa Desemba 10 mjini Oslo, tarehe ya kumbukumbu ya kifo cha Alfred Nobel.

Malala Yousafzaï na Kailash Satyarthi watagawa tuzo hiyoyenye thamani ya Euros 870,000.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana