Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

Hong Kong yapumua baada ya maandamano ya siku kadhaa

Wafanyakazi wa Umma jijini Hong Kong wameanza kurejea kazini leo Jumatatu saa chache kabla ya kufikia tamati makataa iliyotolewa na serikali ya jiji hilo kuwataka kuondoka kwenye maeneo wanayoyakalia.

Polisi ikiingilia kati wakati wa makundi mawili hasimu yaliyokua yakikabiliana baada ya waandamanaji kuweka vizuizi barabarani.
Polisi ikiingilia kati wakati wa makundi mawili hasimu yaliyokua yakikabiliana baada ya waandamanaji kuweka vizuizi barabarani. REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wachache wanaotaka mabadiliko ya demokrasia kwenye jiji la Hong Kong wameendelea kusalia kwenye barabara za jiji la Hong Kong huku wakiwa wameondoa vizuizi kwenye ofisi za serikali.

Hata hivyo licha ya waandamanaji wengi kuondoka kwenye maeneo ya awali waliyokuwa wanayakalia kwa zaidi ya Juma moja, baadhi yao wameapa kurejea tena mchana huu kuendelea na harakati zao za kutaka mabadiliko.

Kiongozi wa jiji la Hong Kong, Leung Chun-ying ambaye ameendelea kukaidi madai ya waandamanaji hao wanaomtaka ajiuzulu, amesisitiza kuwa ni lazima ofisi za Serikali zifunguliwe pamoja na kuruhusu wanafunzi kuendelea na masomo na kuonya kuwa utawala wake utachukua hatua dhidi ya waandamanaji watakaosalia.

Wanaharakati, raia wa kawaida na wanafunzi wa vyuo vikuu wanashinikiza utawala wa Beijing kuruhusu wananchi wa jiji la Hong Kong kuchagua viongozi wao kwenye uchaguzi wa mwaka 2017 badala ya kuchaguliwa na kamati kuu ya jiji la Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.