Pata taarifa kuu
DRC-SIERRA LEONE-EBOLA-

Congo na Liberia zatangaza hali ya hatari kufuatia virus vya Ebola

Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ametangaza alhamisi wiki hii hali ya hatari kufuatia virusi vya Ebola, ambavyo vimesababisha vifo vya watu 224, na kusitisha safari yake nchini Marekani, ambapo angelishiriki mkutano katiya Afrikana Marekani.

Serikali ya Sierra Leone yatangaza hali ya hatari kufuatia virusi vya Ebola.
Serikali ya Sierra Leone yatangaza hali ya hatari kufuatia virusi vya Ebola. Photo: Reuters/Tommy Trenchard
Matangazo ya kibiashara

Rais Koroma amesema wametangaza hali ya hatari ili kutazama jinsi ya kuchukua hatua zinazohitajika dhjidi ya virusi vya Ebola.

Katika kijiji cha Kenema, nchini Sierra Leone, viongozi mbalimbali katika sekta ya afya na serikali wakiendeha zoezi la vipimo vya damu kwa raia, ili kuchunguza iwapo wameambukizwa virusi vya Ebola. le 25 juin 2014.
Katika kijiji cha Kenema, nchini Sierra Leone, viongozi mbalimbali katika sekta ya afya na serikali wakiendeha zoezi la vipimo vya damu kwa raia, ili kuchunguza iwapo wameambukizwa virusi vya Ebola. le 25 juin 2014. REUTERS/Umaru Fofana

Hayo yakijiri, serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imesema imo mbiyoni kuchukua hatua zinazohitajika kiafya ili kudhibiti kutokea kwa virusi vya Ebola kwenye aridhi yake, ambayo imesababisha vifo vya watu 700 katika baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi tangu mwanzoni mwa mwaka.

“Kwa sasa tumechukua hatua, ambazo ni pamoja na ukaguzi na kuwafanyia vipimo vya afya abiria wote wanaowasili kwenye viwanja vya ndege zinazotokea nchini Nigeria”, waziri wa afya, Félix Kabange Numbi amesema.

Virus vya Ebola viligudulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia katika mwaka 1976. Tangu tarehe hiyo, Congo imekua ikishuhudiwa vifo kutokana na virusi vya Ebola. Novemba mwaka 2012, watu 36 walifariki kaskazini mashariki mwa taifa hilo kutokana na virusi hivyo vya Ebola.

Kwa sasa mataifa yanayo kabiliwa na virusi vya Ebola ni Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria , ambapo mtu mmoja alifariki hivi karibuni kutokana na Virusi vya Ebola, baada ya ndege aliyokuemo ikitokea Monrovia kutua katika uwanja wa Lagos. Hali hiyo imepelekea mataifa mawili ya ndege Arik na ASKY kusitisha safari zao nchini Liberia na Sierre Leone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.