Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Ufaransa yaanza vema michuano ya kombe la dunia Brazil, leo ni zamu ya Nigeria na Ghana wawakilishi wengine toka bara la Afrika

Timu ya taifa ya Ufaransa “Les Bleus” imeanza vema michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia nchini Brazil, baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Honduras kwenye mchezo ambao ulikuwa na utata mwingi. 

Karim Benzema, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa
Karim Benzema, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mechi hiyo ambayo toka kipindi cha kwanza timu ya taifa ya Ufaransa ilionesha nia ya kutaka kuchomoza na ushindi dhidi ya mpinzani, ilishuhudia vijana wa kocha Didier Deschamp waking'ara vilivyo kwenye mchezo huu.

Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema
Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema REUTERS/Michael Dalder

Walikuwa ni Ufaransa ambao ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya tuta kwenye dakika ya 45 ya mchezo, bao lililofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji, Karim Benzema ambaye kwenye mechi hii alikuwa mwiba mkubwa kwa Honduras.

Penati hii ilipatikana baada ya mshambuliaji wake, Pogba kuangushwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi Sandro Ricc wa Brazil kuizawadia Ufaransa penati iliyowawezesha kuapata bao la mapema.

Mpaka timu hizi zinakwenda mapumziko, Ufaransa walikuwa wakiongoza kwa bao moja, kipindi cha pili kilianza kwa kasi, ambapo Ufaransa waliendelea kuwabana vijana wa Honduras ambao waliendelea kukubali kucheza kwaride la “La Gaule”.

Ufaransa ilipata bao lake la pili kwenye dakika ya 48 ya mchezo, safari hii beki wa Honduras, N.Valladares akijifunga wakati akijaribu kuonkoa mpira wa krosi ulipigwa kutoka upande wa kushoto.

Benzema aliihakikishia timu yake ushindi wa kwanza kwenye mechi hii ya ufunguzi ya kundi E, baada ya kupachika bao safi kufuatia mpira wa Patrice Evra alioupiga kuwababatiza mabeki wa Honduras ambao walishindwa kuuokoa na kumkuta Karim Benzema aliyeuweka kimiani kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Hinduras.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taufa ya Ecuador, Antonio Valencia
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taufa ya Ecuador, Antonio Valencia REUTERS

Mchezo mwingine kwenye kundi E ulizikutanisha timu ya taifa ya Uswis waliokuwa na kibarua dhidi ya Ecuador kwenye mchezo ambao ulitoa matokeo ya kushangaza baada ya Ecuador waliokuwa mbele kwa bao moja kukubali bao hilo kurejeshwa na Uswis kupata bao la ushindi.

Mchezo kati ya Ecuador na Uswis ulikuwa wa upinzani mkali kwa muda wote wa mchezo, ambapo timu zote mbili zilikuwa zikifanya mashambulizi kwa zamu na yakushtukiza kutaka kutafuta mabao zaidi.

Ecuador ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao kwenye dakika ya 22 ya mchezo, bao lililofungwa na mchezaji Enner Valencia aliyeutumia vema mpira wa pasi aliopigiwa na mchezaji, W.Ayovi.

Timu hizi zilienda mapumziko Ecuador wakiwa wanaongoza kwa bao moja, kipindi cha pili kilianza kwa kasi, ambapo Uswis walizidisha mashambulizi yaliyozaa matunda katika dakika ya 48 baada ya mchezaji Mehmedi kuisawazishia timu yake bao akitumia vema pasi ya Rodriguez.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uswis
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uswis fifa.com

Uswis walihitimisha furaha ya ushindi kwa bao la Seferovic katika dakika ya za nyongoza akitumia uzembe wa mabeki wa Ecuador waliojisahau na kuruhusu mpira kukaa sana kwenye eneo la la haari na kumpa mwanya mchezji huyu kupachika bao la ushindi kwa timu yake.

Hapo jana pia kulikuwa na mchezo mmoja tu wa kundi F lenye timu za, Argentina, Bosnia, Iran na Nigeria.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Bosnia wakishangilia moja ya mabao waliyofunga wakati wa michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia Brazil 2014
Wachezaji wa timu ya taifa ya Bosnia wakishangilia moja ya mabao waliyofunga wakati wa michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia Brazil 2014 fifa.com

Argentina wakiongozwa na nahodha Lionel Messi walitupa karata yao ya kwanza dhidi ya wageni wa michuano ya mwaka huu, Bosnia, kwenye mchezo ambao licha ya ushindi wa mabao 2-1 iliyoupata Argentina, Bosnia haikuwa timu ya kubeza kwakuwa nao walijitutumua kutaka kusawazisha na pengine kupata ushindi.

Argentina ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya mchezaji wa Bosnia, Sead Kilasinic kujifunga akiwa kwenye harakati za kutaka kuokoa mpira wa krosi, na badala yake akabadili uelekeo wa mpira uliomshinda mlinda mlango wake.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi alishangilia moja ya bao alilofunga dhidi ya Bosnia
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi alishangilia moja ya bao alilofunga dhidi ya Bosnia fifa.com

Argentina waliandikisha bao lao la pili kwenye dakika ya 65 ya mchezo likufungwa na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Bosnia kwa kuwapiga chenga na kisha kupiga shuti lililotinga moja kwa moja kwenye kimia.

Bosnia walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi katika dakika ya 84 ya mchezo likifungwa na Vedad Ibisevic kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Senad Lulic aliyetoa pasi ya uhakika kumkuta mfungaji.

Nhodha wa Ghana, Asamoah Gyan akiwa mazoezini
Nhodha wa Ghana, Asamoah Gyan akiwa mazoezini REUTERS/Toru Hanai

Leo pia kutakuwa na mechi kadhaa ambapo wawakilish wengine wa Afrika timu ya taifa ya Nigeria “Super Eagles” watakuwa na kibarua dhidi ya Iran kwenye mchezo wa kundi F, huku kwenye kundi G kukiwa na mchezo mwingine utakao zikutanisha timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Ureno, huku wawakilishi wengine wa Afrika timu ya taifa ya Ghana wao watatupa karata yao siku wa manane kwa saa za hapa Afrika Mashariki dhidi ya Marekani.

Timu pekee ya Afrika iliyopata ushindi ni Ivory Coast ambayo ilishinda kwenye mchezo wao wa awali dhidi ya Japan, huku Cameroon wao wakipoteza mchezo wa awali kwa kukubali kufungwa na Mexico kwenye mchezo wa kundi A.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.