Pata taarifa kuu
Pakistani-Taliban

Jeshi la Pakistani lazima shambulio la Taliban mjini Karachi

Viongozi nchini Pakistan wametangaza wamefaanikiwa kuzima shambulio kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Karachi nchini Pakistan baada kundi la wanamgambo wa Taliban kushambulia kwa muda wa saa kumi na mbili na kusababisha vifo vya watu 28 wakiwemo waasi 10. Shambulio hilo la wanambgambo wa Taliban ni ishara tosha ya udhaifu wa vikosi vya usalama katika kulinda vituo muhimu husasan ambavyo vinatakiwa kuwa na ulinzi mkali.

Moshi ukionekana kwenye uwanja wa ndege wa Karachi baada ya kuzimwa kwa shambulio Juni 9, mwaka 2014
Moshi ukionekana kwenye uwanja wa ndege wa Karachi baada ya kuzimwa kwa shambulio Juni 9, mwaka 2014 REUTERS/Athar Hussain
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo kubwa kuwahi kushuhudiwa katika mji huo wa kiuchumi nchini Pakistan, umesababisha shuhguli zote za usafiri wa ndege kupwaya kuanzia jana Jumapili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah.

Hata hivyo shughuli hizo zinataraji kuanza tena baade jioni hii kulingana na msemaji wa mamlaka ya shughuli za usafiri wa angani Abid Ali Khan.

Kundi la Taliban kutoka Pakistan la TTP limefanya shambulio ambalo lilianza tangu saa kumi na mbili jioni saa za kimataifa na kusitishwa saa kumi na mbili baadae pale  kikosi maalum cha jeshi kuingilia kati na kuwauawa wapiganaji 10 wa Taliban.

Kikosi cha polisi ya usalama kikiwa nje ya uwanja wa ndege wa Karachi baada ya kuzimwa kwa shambulio la watu waliokuwa na silaha Jumapili Juni 8, mwaka 2014
Kikosi cha polisi ya usalama kikiwa nje ya uwanja wa ndege wa Karachi baada ya kuzimwa kwa shambulio la watu waliokuwa na silaha Jumapili Juni 8, mwaka 2014 PHOTO/Asif HASSAN

Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa jeshiSibtain Rizvi amesema wamezima shambulio na wamefaanikiwa kuwauawa washambuliaji wote walioendesha shambulo hilo.

Shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 28 wakiwemo waasi 10, na wafanyakazi wa uwanja wa ndege.

Kundi la TTP linaendesha mashambulizi tangu mwaka 2007 dhidi ya serikali ya Islamabad inayotuhumiwa na kundi hilo kuwa ya kimagharibi.

Akijigamba kundi lake kuhusika na shambulio hilo, msemaji wa kundi hilo Shahidullah Shahid amesema shambulio hilo linalenga kulipiza kisase dhidi ya kifo cha kiongozi wao Hakimullah Mehsud aliye uawa siku za hivi karibuni na shambulio la ndege zisizokuwa na rubani za Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.