Pata taarifa kuu
CHAD-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Chad yajitetea kuhusu kuondoa wanajeshi wake Jamhuri ya Afrika ya Kati

Serikali ya Chad imechukua uamzi wa kuondoa wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikibaini kwamba imeepuka mauaji dhidi ya raia wake waliyokua wakilengwa pamoja na wanajeshi wake.

Mwanajeshi kutoka Chad katiaka barabara ya mji wa Bangui.
Mwanajeshi kutoka Chad katiaka barabara ya mji wa Bangui. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

“Uamzi wa Chad wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati unapaswa kutekelezwa, kwani raia wa taifa hili na wanajeshi wake walioko nchini humo wamekua wakilengwa, amesema waziri wa mambo ya nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat.

Mahamat amebaini kwamba Chad haiwezi kufumbia macho wanajeshi wake waendeleye kuuawa halafu wasijihami. Amesema kamwe serikali ya Chad haiwezi kukubaliana na hali hio. Mahamat amesema kwamba wanajesshi hao wataondoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hatua kwa hatua.

Uamzi huo wa kuondoa wanajeshi 850 wa Chad nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, unakuja baada ya raia 24 kuuawa mwishoni mwa juma liliyopita na wanajeshi wa Chad.

Tukio hilo linalohusisha kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya kigeni ni kubwa kuwahi kutokea nchibni Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu, alipopinduliwa madarakani rais François Bozizé na waasi wa kundi la Séléka, mwezi machi mwaka 2013. Waasi hao wa Séléka walikua wakiungwa mkono na nchi ya Chad.

Kwa mujibu wa Mahamat, wanajeshi wa Chada walijihami, baada ya kushanbuliwa kwa risase na wanamgambo wa kundi la wakristo la ant-balaka, akibaini kwamba ni kawaida kujihami unaposhambuliwa.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Chad kunakuja wakati Ufaransa, Umoja wa Mataifa hata viongozi wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameomba idadi ya wanajeshi kutoka mataifa ya kigeni iongezwe ili kudumisha amani, hususan katika mkoa wa mashariki, ambapo wanajeshi wa Ufaransa wameanza kuondolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.