Pata taarifa kuu
Kenya-mauaji

Polisi jijini Mombasa waimarisha usalama baada ya mauaji ya cheikh Abubakar Shariff, maharufu Makaburi

Polisi kwenye mji wa Mombasa hii leo wameendelea kuimarisha usalama kwenye mji wa Mombasa kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa dini ya kiislamu Cheikh Abubakar Shariff Ahmed, maharufu kama Makaburi, jana usiku na watu wasiojulikana, tukio ambalo limewashtua wengi.

Abubakar Shariff Ahmed wakati wa uhai wake
Abubakar Shariff Ahmed wakati wa uhai wake Aljazeera
Matangazo ya kibiashara

Sheikh Abubakar Shariff Ahmed alikuwa ni moja kati ya viongozi waliokuwa wakimuunga mkono Osama Bin Laden na alikuwa kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa UN kwa tuhuma za kuwa mstari wa mbele kutoa msaada na mafunzo kwa vijana wa Kenya kujiunga na kundi la Al-Shabab nchini Somalia.

Hali ya utulivu iliripotiwa kwenye maeneo mengi ya mji wa Mombasa wakati huu kukiwa na hofu ya kiusalama hasa kwa vijana ambao walikuwa wafuasi wa karibu wa Sheikh Ahmed aliyefahamika pia kwa jina la Makuburi.

Kumeibuka maswali kuhusu ni nani hasa aliyehusika na kifo cha kiongozi huyu na kama ni muendelezo wa mauaji ya viongozi wa kidini waliomstari wa mbele kuunga mkono sera za Al-Shabab na Al-Qaeda nchini Kenya?

Wito wa utulivu umeendelea kutolewa kwenye vipaza sauti vya Muskiti Musa usiku kucha pamoja na radio za eneo hilo huku idadi kubwa ya polisi wakimiminika katika maeneo mbalimbali hususan makanisani pamoja na eneo la Muskiti wa Masjid Musa.

Vifo vya maiamamu Aboud Rogo Mohamed aliyekuwa akihubiri katika Masjid Musa ambaye alipigwa risase Agosti mwaka 2012, pamoja na mauaji ya mrithi wake Ibrahim Ismail yaliotekelezwa mwaka 2013, yalizua mara kadhaa hali ya sintofahamu katika mji wa Mombasa ambapo wafuasi wa viongozi hao waliokuwa wakiongozwa na Makaburi waliituhumu serikali ya Kenya kuhusika na mauaji hayo.

Wizara ya mambo ya nje nchini Uingereza imetowa wito kwa watu wanaofanya ziara katika eneo hilo kuwa makini zaidi katika kipindi hiki ambapo mauaji ya kiongozi huyo huenda ikazua taharuki zaidi.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.