Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Ufilipino imepiga hatua katika mchakato wa amani

media Wanawake kutoka jamii ya Moro, katika eneo la Pikit, katika mkoa wa Cotabato, wanasheherekea kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya waasi na serikali, alhamisi machi 27. REUTERS/Keith Bangcoco

Waasi wa kiislamu nchini Ufilipino wamesaini jana kwenye ikulu mjini Manila mkataba wa amani na wawakilishi wa serikali ya Ufilipino. Pande hizo mbili zimekubaliana kuundwa na kujitegemeya kwa jimbo la Bangsamoro. Mkataba huo unakuja kumaliza machafuko yaliyosababisha watu 150.000 kupoteza maisha tangu machafuko hayo yalipoanza mwaka 1970.

Jimbo la Bangsamoro litaundwa na mikoa mitano inayopatikana ndani na pembezuni mwa kisiwa cha Mindanao, kusini mwa nchi, sawa na asilimia 10 ya nchi nzima.

Jimbo la Bangsamoro litakua na bunge lake pamoja na wanajeshi wake, huku likiingiza moja kwa moja katika hazina yake asilimia 75 ya ushuru na kodi na kumiliki asilimia 75 ya mapato ya maliasili, hususan madini.

Katika masuala ya dini, sheria za kiislamu zimepewa kipaumbele kwa kutatua mizozo katika jamii ya waislamu. Mji mkuu wa Manila utabaki na majukumu ya kitaifa, hususan ulinzi, ushirikiano wa kimataifa, fedha na uzalendo.

Inatakiwa miaka miwili, iwapo mambo yataenda vizuri, ili mchakato uwe umekalimika. Rais wa Ufilipino Aquino anatakiwa kabla ya mwisho wa mwaka huu, kuwasilisha nyaraka za kujitegemea kwa jimbo la Bangsamoro mbele ya bunge na baraza la katiba. Mwaka 2015 raia kutoka mikoa husika wataitishwa katika upigaji kura ya maoni.

Ni kwa wakati huo serikali ya mpito itakapoteuliwa, kwa kusubiri uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2016 utakaowachagua wabunge 50.

Makundi ya kislamu ya kusini mwa Ufilipino yalijitenga na utawala wa Manila tangu miaka ya 1960, huku kundi la waasi wa kiislamu la FMLN likianzisha harakati zake za kijeshi katika mwaka 1969.

Ni miaka 45 sasa, tangu kuweko na mazungumzo, usitishwaji mapigano, na mikataba bila hata hivo kutokomesha machafuko.
 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana