Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Jeshi la Israel laendesha mashambulizi nchini Syria

media Mwanajeshi wa Israel aliejeruhiwa jana jumanne machi 18 mwaka 2014 kwenye mlima wa Golan katika mlipuko wa bomu liliyotengenezwa kienyeji. REUTERS/Gil Nechushtan

Jeshi la Israel limejibu usiku wa jana kuamkia leo shambulizi la bomu liliyotengenezwa kienyeji kwenye mlima wa Golan, na kuwajeruhi wanajeshi wanne wa Israel. Maeneo mengi ya jeshi la Israel yalikua yamelengwa na mashambulizi yaliyokua yamepangwa na makundi yanayoendesha shughuli zao nchini Syria.

Ilikua karibu na majira ya alfajiri saa za Syria, wakati ndege za Israel zimeendesha mashambulizi manne mfululizo nchini Syria. Ndege hizo zimeendesha mashambulizi hayo katika maeneo manne muhimu ya kijeshi, kambi ya mazoezi ya kijeshi na ngome za kijeshi, taarifa hio ni kwa mujibu wa jeshi la Israel.

Haijafahamika hadi sasa hasara za mashambulizi hayo. Jeshi la Israel limebaini kwamba imejibu shambulizi la jana katika eneo la Golan, katika mpaka na Syria.

Imekua ni shambulizi la tatu tangu mwezi wa machi, lakini shambulizi hili limekua kubwa zaidi.

Waziri mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu, ameonya jana jioni kwamba watajibu kijeshi kwa wakati wowote ule, akinyoosheya kidole vitisho kundi la Hezbollah, ambalo ni mshirika wa karibu wa Syria, lakini pia makundi ya waislamu wenye msimamo mkali.

Hali ya sintofahamu inajiri wakati huu kati ya Syria na Israel.

 

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana