Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/11 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/11 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 19/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Israeli yadai kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Syria
 • Papa Francis awasili Thailand, hatua ya kwanza ya ziara yake barani Asia
Asia

Malaysia : Uchunguzi wa ndege ya Malaysia Airlines iliyopotea unaendelea

media Mmoja kati ya wataalamu kutoka nchini Vietnam wakiendelea na uchunguzi kuhusu kupotea kwa ndege ya Malaysia Airlines. EPA

Wataalamu wanaoendesha uchunguzi kuhusu ndege ya Malaysia Airlines iliopotea siku sita zilizopita baada ya kupoteza mawasiliana wanasema hakuna dalili zozote za kutokea mlipuko ikiwa angani wakati huu Satalite za China zikigundua vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni kutoka katika ndege hiyo.

wataalamu wa China wamesema moja kati ya satalite kumi walizotuma kutafuta mabaki ya ndege hiyo wamegunduwa vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni vya watu waliokuwemo katika ndege hiyo iliotoweka tangu siku ya Jumamosi.

Operesheni hiyo ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo zimepanuliwa zaidi katika bahari ya Andaman katika eneo la magharibi mwa Malaysia mbali kidogo na eneo ambalo ndege hiyo inashukiwa huenda ndiko iliko angukia ikiwa na abiria 239.

Tayari Malaysia imetuma ndege zake katika eneo la anga ambalo satalite za China zimegunduwa mabaki ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya watu waliokuwemo katika ndege hiyo.

Wakati huo huo wataalamu wa Marekani wamesema hakuna viashiria vyovyote vinavyoonyesha kuwa kulitokea mlipuko katika ndege hiyo wakati ikiwa angani kabla ya kuanguka.

Ndege hiyo ya Malaysia iliokuwa ikisafiri kutoka jijini Kualalumpur kuelekea jijini Pekin nchini China ilipotea kimiujiza ikiwa angani na watu 239, huku wengi wao wakiwa ni raia wa China.

Zaidi ya nchi tisa zinashiriki katika opereshani ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo ambapo hadi sasa juhudu hizo hazijazaa matunda.
 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana