Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Diplomasia

Serikali ya Sudan Kusini yaonya Jumiya ya IGAD kutoingilia mamlaka yake

Wakati viongozi wa nchi za Jumuiya ya IGAD zikitarajiwa kuanza mkutano wake mjini Juba, serikali ya Sudan Kusini inasema kuwa kamwe haitakubali kuona mamlaka yake kama nchi yanaingiliwa na mtu yeyote.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir RFI
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Sudan Kusini inatolewa wakati huu mazungumzo ya amani kati yake na ujumbe wa aliekuwa makamu wa rais wa taifa hilo, Riek Machar yakiendelea mjini Addis-Ababa ambako wanatarajiwa kuja na maazimio ya kusitisha mapigano nchini humo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Amina Mohamed ambae anahudhuria mkutano wa nchi wanachama za IGAD, anasema kuwa baraza la usalama limeidhinisha kikosi cha zaidi ya wanajeshi elfu 5 kupelekwa nchini humo kulinda usalama chini ya makubaliano na serikali ya Juba.

Kwa upande wake serikali ya Sudan Kusini inasema kuwa wako tayari kuona wakisitisha mapigano nchini humo lakini hawako tayari kuamuliwa nini chakufanya kuhusu hatua za kuchukua ili kuleta maridhiano na usitishwaji wa mapigano.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa nchi wanachama wa Jumuiya mbalimbali barani Afrika lazima waungane na kuwa na msimamo mmoja kuhusu kushughulikia mzozo wa nchi ya Sudan Kusini.

Juma hili nchi wanachama za IGAD ziliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa UN la kutuma wanajeshi zaidi ya elfu 5 na 500 kwenda nchini Sudan Kusini kuongeza nguvu kwa vikosi vingine vya Umoja wa mataifa vilivyoko nchini humo.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa bado viongozi wengi wanatofautiana kimtazamo kuhusu namna ya kushughulikia mzozo wa taifa hilo kwakuwa kuna baadhi zimeshatuma wanajeshi wake hata kabla ya vile vikosi vya Umoja wa mataifa na kwamba ni lazima waje pamoja na kutoa msimamo unaoeleweka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.