Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Uhalifu dhidi ya ubinadamu waripotiwa nchini Sudan Kusini

media Mjumbe maalumu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Ivan Simonovic … RFI

Mjumbe maalumu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Ivan Simonovic amesema ameona miili iliyofungwa kwa pamoja na kupigwa risasi katika miji mbalimbali nchini Sudan Kusini,  akibaini kwamba watalaamu 92 wa haki za Binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wapo nchini humo kuendeleza uchunguzi wake na watatoa ripoti yao kwa kipindi cha wiki mbili zijazo.

Umoja wa Mataifa unamtuhumu rais Salva Kirr na aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar kwa kutekeleza mauji makubwa na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za Binadamu kupitia vikosi vyao.

Jeshi la Uganda la UPDF limekiri kukabiliana na waasi wa Riek Machar wakati huu na hivi karibuni wanajeshi kadhaa wa uganda walipoteza maisha na waasi wengi wa Uganda waliuawa.

Uwepo wa majeshi ya Uganda upande wa serikali ya Juba, unapelekea hali ya mazungumzo huko Ethiopia kuendelea kupwaya. Kufuatia vile Uganda ni mwanachama wa Igad na sasa anaegemea upande mmoja.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa wanaona kuwa Igad imeshindwa, na sasa Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuingilia kati.
 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana