Pata taarifa kuu
KENYA

Watano wapoteza maisha katika mlipuko Pangani Kenya

Takribani watu watano wamethibitika kupoteza maisha huku idadi ikihofiwa kuongezeka baada ya kutokea mlipuko uliojeruhi wengine 36 jumamosi nchini kenya.

Magari ya msalaba mwekundu yakiwa eneo la tuukio tayari kutoa msaada baada ya shambulizi la kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu
Magari ya msalaba mwekundu yakiwa eneo la tuukio tayari kutoa msaada baada ya shambulizi la kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu
Matangazo ya kibiashara

Bado ni muendelezo wa mashambulizi yasiyoeleweka nani anayehusika huku ikishuhudiwa watu 13 wakipoteza maisha tangu jumanne juma hili.

Mkuu wa polisi jijini Nairobi Benson Kibue amesema uchunguzi unafanyika kubaini ni aina gani ya bomu ilitumika kusababisha madhara yaliyojitokeza na ikiwa mshambuliaji alikuwa miongoni mwa abiria wa matatu hiyo au la.

Kwa mujibu wa polisi gari hiyo matatu hiyo ililipuka eneo la pangani baada ya kutoka eneo la jirani na nairobi isti lii eneo ambalo imejaa jamii ya wasomali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.