Pata taarifa kuu
DRC

Wapiganaji wa Mai Mai walioweka silaha chini waanza kupatiwa mafunzo ya kijeshi chini ya usimamizi wa Serikali ya DRC

Wapiganaji wa Mai-Mai waliojisalimisha na kuweka silaha chini jimboni Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameanza kupatiwa mafunzo ya kuwa askari chini ya uongozi wa serikali.

Baadhi ya wapiganaji walioweka silaha chini huko Mashariki mwa DRC
Baadhi ya wapiganaji walioweka silaha chini huko Mashariki mwa DRC RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Rishali Muyeji ametembelea takribani vijana elfu moja na mia mbili kando ya mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo ambao wameanza kupatiwa mafunzo hayo.

Waziri Muyeji aliyewatembelea vijana hao kwenye mji wa Bweremana Magharibi mwa Goma amewapongeza kwa kuitika wito wa raia na serikali ya Congo kwa uamuzi wa kuacha uasi na kuweka silaha chini.

Aidha vijana hao baada ya kuacha uasi wametoa mahitaji yao kwa waziri Muyeji kuwa wanahitaji mavazi, mahali pa kulala na chakula jambo ambalo waziri amesema kuwa rais Kabila ameandaa mpango wa kuhakikisha wanapata mahitaji hayo.

Hadi sasa jumla ya vikundi ishirini na tano vimetoa watu takribani 1002 kujiunga na kambi ya mafunzo ya kuwa raia wa kawaida ama kujiunga na jeshi huku vikundi vingine navyo vikiendelea kuweka silaha chini.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.