Pata taarifa kuu
TANZANIA-Siasa

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA,Chawavua nyadhifa Zitto Kabwe na Mkumbo Kitila

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA,kimetangaza kuwavua madaraka yao yote mbunge wa kigoma kaskazini kupitia chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Mkumbo Kitila.

Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA,Willbroad Slaa
Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA,Willbroad Slaa dar24.com
Matangazo ya kibiashara

Kwenye maamuzi hayo kamati kuu imesema kuwa Zitto na kitila wanatuhumiwa kwa kufanya harakati za kutaka kukihujumu chama hicho pamoja na kwenda kinyume na maamuzi ya chama na mwenendo wake.

Akizungumza na rfikiswahili katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Willbroad Slaa amesema hata kama mtu ataamua kuondoka ndani ya chama hicho,kamwe hakitatetereka.

Kwa uamuzi huo sasa Zitto amepoteza nafasi yake ya unaibu katibu mkuu na unaibu mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, huku mkumbo Kitila yeye akivuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu ya chama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.