Pata taarifa kuu
USWISI-Mazungumzo ya Nyuklia

Matokeo ya mazungumzo ya nyuklia nchini Uswisi hayatabiriki

Wanadiplomasia wa nchi tano zenye nguvu duniani wameingia katika siku ya tatu ya majadiliano na serikali ya Iran kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran wakati ambapo kukiwa na utata juu ya maswala nyeti.

Wajumbe kutoka, Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani wanaingia siku ya tatu ya  majadiliano na Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia
Wajumbe kutoka, Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani wanaingia siku ya tatu ya majadiliano na Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia AFP PHOTO / OZAN KOSE
Matangazo ya kibiashara

Duru za kidiplomasia kutoka Umoja wa Ulaya zimearifu kwamba siku hii inaweza kuwa ya maamuzi, licha ya kwamba katika jopo la mabalozi waliopo mjini Geneva hakuna anayeweza kutabiri matokeo ya mazungumzo hayo na lini yatafikia kikomo.

Hapo jana naibu waziri wa mambo ya ndani wa Iran katika mazungumzo hayo Abbas Araghachi amesema licha ya kuwa na mazungumzo yenye tija na ujumbe unaongozwa na mkuu wa sera za mambo ya nje kwenye Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton, bado kuna masuala nyeti ambayo yameendelea kuwa tata kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Mapema hii leo asubuhi Catherine Aston anakutana na kiongozi wa ujumbe wa Iran kwenye majadiliano hayo Javad Zarif kabla ya kutoa ripoti kwa wajumbe kutoka, Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani kabla ya kuingia ndani zaidi kwenye majadiliano.

Mapema alhamisi Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Geneva Abbas Araghachi alionya juu ya kutokuaminiana kama moja ya kikwazo cha mazungumzo hayo yahusuyo nyuklia kati ya mataifa makubwa duniani na nchi ya Iran.

Kikwazo cha kutoaminiana kimekuwa kikubwa hasa katika majadiliano ya mwisho na kuona kuwa ikiwa suala la kukosekana kwa kuaminiana haitawezekana kuendelea na mazungumzo yenye tija kama alivyonukuliwa Abbas Araghachi akisema katika televisheni ya taifa hilo.

Hata hivyo Wachambuzi wa siasa wanaonakuwa hakuna matumaini yoyote ya kupatikana muafaka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.