Pata taarifa kuu
PALESTINA

Ripoti ya uchunguzi yabaini huenda Rais wa zamani wa mamlaka ya Palestina, Yasser Arafat aliuawa kwa sumu

Ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa kwa familia ya Rais wa zamani wa mamlaka ya Palestina marehemu Yasser Arafat imeonesha kuwa huenda kiongozi huyo aliuawa kwa kutumia sumu ya Polonium 210. Wataalamu wa mionzi nchini Uswisi wamebaini kuwemo kwa kiasi kikubwa cha sumu ya Poloniam kwenye mabaki na nguo za Arafat kiwango ambacho wanadai si cha kawaida.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na kituo cha kiarabu cha Al-Jazeera mjane wa Arafat, Suha Arafat ameeleza kushtushwa na ripoti hiyo na kudai kuwa yeye na mwanawe hawatakaa kimya mpaka pale wale waliohusika watakapofikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ripoti ya wataalamu wa Uswiss ni ya kwanza kati ya ripoti nyingine mbili zinazosubiriwa kutolewa na wataalamu wa Ufaransa na wale wa Urusi ambao ripoti yao imedokeza kutokuwemo kwa kiasi chochote cha sumu ya Polonium.

Arafat aliuawa nchini Ufaransa mwezi Novemba mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 75 lakini madaktari walishindwa kubaini sababu za kifo chake.

Sampuli za mabaki ya mwili wake zilichukuliwa mwaka 2012 na uchunguzi ulifanyika ili kubaini iwapo aliuawa, hatua hiyo iliibuka baada ya kifo cha jasusi wa zamani wa Urusi, Alexander Litvinenko aliyeuawa jijini London mwaka 2006.

Israel imekuwa ikishutumiwa kuhusika na mauaji ya Rafat, na imekuwa ikikanusha madai hayo na tayari Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imetupilia mbali matokeo ya uchunguzi wa wanasayansi na kusema hauna ukweli wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.