Pata taarifa kuu
UMOJA WA MATAIFA UN-UMOJA WA AFRIKA-AU

Umoja wa Mataifa,Bank ya Dunia kupambana na umasikini nchini Mali

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Mkuu wa banki ya dunia Jim Yong Kim wanatarajia kuanzisha harakati za kukabiliana na umasikini nchini Mali na mataifa mengine manne barani Afrika juma lijalo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu Ban, kiongozi wa banki ya dunia Kim,viongozi wa juu katika Umoja wa Afrika,banki ya maendeleo ya Afrika na Umoja wa Ulaya watakutana nchini Mali juma lijalo na baadaye wataelekea Niger, Burkina Faso na Chad.

Kuhusu mgogoro wa Mali katibu wa UN Ban Ki Moon alisema kuwa kipindi ambacho waasi wa kiislamu walipodhibiti eneo la kaskazini mwa nchini hiyo ni takribani mwaka na kusisitiza haja ya kuchukua hatua zaidi ya kupambana katika kanda hiyo ili kuondoa matatizo yanayoweza kuibua mgogoro na kukosekana kwa usalama.

Takribani watu milioni 11 kati ya milioni 80 wanaoishi katika pwani ya Afrika magharibi wanakabiliwa na uhaba wa chakula,huku kanda hiyo ikishuhudia ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.