Pata taarifa kuu
ISRAEL-SYRIA

Ndege za kivita za Israel zatekeleza mashambulizi ya angaa nchini Syria

Ndege za kivita za Israel limetekeleza mashambulizi ya angaa karibu na mji wa Latakia Pwani ya Syria.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi Israel halijazungumzia lolote kuhusu oparesheni hii lakini ripoti zinasema mashambulizi hayo yalilenga kuharibu silaha hatari zinazoaminiwa kutengezwa  nchini Urusi na zilikuwa zinasafirishwa nchini Lebanon kulifikia kundi la Kislamu la Hezbollah ambalo linasalia hatari kwa usalama wa Israel.

Hili ni shambulizi la tatu kufanywa na jeshi la Israel katika mji huo wa Latakia mwaka huu katika ngome hiyo ya wafuasi wa rais Bashar al Assad.

Israel imekuwa ikisema kuwa itaishambulia Syria ikiwa itahisi kuwa silaha zake zinahatarisha usalama wa taifa lao au zinafikia kundi la kiislamu la Hezbollah.

Shambulzi hili linakuja siku moja baada ya Shirika la Kimataifa linaloshughulika na silaha za Kemikali duniani OPCW kusema kuwa limeharibu vifaa vyote vinavyotumiwa kutengeneza silaha za kemikali nchini  Syria.

OCPW lilitoa kauli  hiyo siku moja kabla ya siku ya mwisho ya tarehe 1 mwezi Novemba  iliyokuwa imepangwa na shirika hilo kuharibu viwanda vyote vya kutengeneza silaha hizo hatari.

Mpango wa kuharibu silaha za kemikali za serikali ya Syria ulikubaliwa kati ya serikali ya Marekani na Urusi kama njia mojawapo ya kumaliza mzozo huo na kuzuia uwezekano wa Damascus kuendelea kutumia silaha hizo kuwashambulia raia wake.

Serikali ya Syria sasa ina hadi katikati ya mwaka ujao kuteketeza silaha zake zote za kemikali ambazo ni zaidi ya Tani 1,000.

Mwezi Agosti mwaka huu, serikali ya rais Assad ilitumia kutumia silaha hizo kuwashambulia wapinzani karibu na mji wa Damascus shambulizi ambalo lilisababisha Marekani kutishia kuishambulia Syria kijeshi.

Katika hatua nyingine, rais  Bashar Al Assad amesema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya amani na wapinzani iwapo tu mataifa kutoka nje hayataingilia katika mchakato huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.