Pata taarifa kuu
MALI

Rais wa Mali Keita avunjilia mbali Kamati ya Mabadiliko ya Jeshi iliyokuwa inaongozwa na Kepteni Sanogo

Rais Mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita maarufu kwa jina la IBK amevunjilia mbali Kamati maalum ya Mabadiliko ya Jeshi nchini humo akisema amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Rais wa Mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta amevunjia mbali Kamati ya Mabadiliko ya Jeshi
Rais wa Mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta amevunjia mbali Kamati ya Mabadiliko ya Jeshi REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo iliyokuwa inaongozwa na Kiongozi wa Mapinduzi Kapteni Amadou Haya Sanogo pamoja na wanajeshi wengi walioshiriki kuiangusha Serikali ya Rais Amadou Toumani Toure kitu kilichochangia kuibuka kwa machafuko katika nchi hiyo.

Rais Keita amesema hawezi kuvumilia pale ambapo kuna watu watovu wa nidhamu hivyo ameona bora avunje mbali kamati hiyo kwa sababu imeshindwa kufanyakazi yake kama ilivyopaswa.

Kiongozi huyo wa Mali amesema uchunguzi unafanyika kubaini kwa nini Kamati hiyoimeshindwa kufanyakazi yake ipasavyo na yoyote ambaye atapatikana na hatia ya kutenda kosa atakabiliwa na adhabu.

Keita amesema hatua ya wanajeshi kufanya mgomo mapema juma hili ni kitu ambacho hakiwezi kuvumiliwa hata kidogo na kinaonekana kuchochewa na kamati iliyopewa jukumu la kuhakikisha kuna mabadiliko jeshini.

Rais Keita ambaye amejiapiza kufanya kila linalowezekana katika kuhakikisha anajenga Jeshi imara litakalokuwa nakibarua cha kuimarisha hali ya usalama amesema hatoweza kukaa kimya pale atakapoona juhudi zake zinasitishwa.

Mgomo wa wanajeshi nchini Mali unatajwa kuchangiwa pakubwa na mashambulizi yaliyofanywa na Wapoganaji wa Kundi la Wanamgambo wa Tuareg MNLA Kaskazini mwa Mji wa Kidal.

Katika hatua nyingine Serikali ya Mali imewaachia huru wafungwa ishirini na watatu waliokamatwa mateka kwenye mapigano yaliyotokea Kaskazini mwa Taifa hilo wakati jeshi likipambana na Waasi.

Wizara ya Haki na Sheria imesema uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mazungumzo baina ya serikali na waasi yaliyofanyika nchini Burkina Faso ambapo pande hizo mbili zilikubaliana na kuachiwa kwa mateka hao.

Mwishoni mwa mwezi uliopita Waaso wanaotaka kujitenga kwa eneo la Kaskazinki mwa Mali walitangaza kujiondoa kwenye mazungumzo na Serikali kutokana na kuituhumu kushindwa kuheshimu mkataba wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.