Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC lataka Mashirika ya Misaada ya Kimataifa yaruhusiwe kuingia nchini Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC limetoa wito kwa Serikali ya Syria na Makundi yote ya Upinzani nchini humo kuhakikisha yanatoa nafasi kwa Mashirika ya Kutoa Misaada kuweza kuwafikia watu wanaohitaji huduma yao. Taarifa ya Baraza la Usalama imeeleza kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha mipaka ya nchi ya Syria inafunguliwa ili kuwe na urahis wa kutolewa kwa misaada kwa watu wenye mahitaji walioathiriwa na machafuko yanayoendelea.

Msafara wa magari ya Mashirika ya Kimataiya ya Misaada yakiwa njiani kuelekea nchini Syria
Msafara wa magari ya Mashirika ya Kimataiya ya Misaada yakiwa njiani kuelekea nchini Syria
Matangazo ya kibiashara

Hili ni ombi la pili la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kwa Serikali ya Syria na pande zote zinazopambana kuhakikisha wanatoa nafasi kwa Mashirika ya Kutoa Misaada kuweza kuwafikia waathirika wa machafuko.

Serikali ya Syria imeruhusu Mashirika kumi na mawili pekee ya Kimataifa kufanya kazi ya kutoa misaada kwa wananchi walioathirika ndani ya mipaka yake idadi inayoonekana ni ndogo na Baraza la Usalama.

Wanachama kumi na watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC wameafikiana huu ni wakati wa kuruhusu Mashirika ya Misaada kuwafikia wananchi walionasa kutokana na vita vinavyoendelea nchini Syria.

Baraza la Usalama kwenye taarifa yake limeoneshwa kuguswa na ongezeko la wakimbizi wanaotajwa kufikia zaidi ya milioni mbili kutoka Syria wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Machafuko ya nchini Syria yamedumu kwa miezi thelathini na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja na elfu kumi kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa UN unaotaka kupatikana kwa suluhu ya machafuko hayo.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohusika na Misaada ya Kibinadamu Valerie Amos amesema wakati umefika kwa Baraza la Usalama kufanya kila linalowezekana ili kuhakikishwa misaada inawafikia waathirika ndani ya mipaka ya Syria.

Amos anakiri kuna maelfu ya wananchi wanaohitaji misaada ya haraka nchini Syria kutokana na kupata madhara makubwa yanayochangiwa na vita vilivyodumu kwa kipindi cha miezi thelathini.

Serikali ya Syria yenyewe imesema itafanyia kazi azimio hilo la Baraza la Usalama kabla haijatoa jibu la kuruhusu mashirika hayo au kluyapinga kwani wanafanya tathmini ya madhara yanayoweza kupatikana.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Bashar Jaafar amesema watakaa chini na kujadili azimio hilo huku wakiangalia namna ambavyo wanaweza wakafanya ili misaada hiyo isije ikawa njia ya kupenyeza silaha kuelekea kwa waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.