Pata taarifa kuu
MAREKANI

Rais Obama asitisha ziara yake ya Malaysia ili apate muda wa kushawishi kupitishwa kwa Bajeti Mpya

Rais wa Marekani Barack Hussein Obama amelazimika kufuta safari yake ya kikazi nchini Malaysia kutokana na kuhitaji muda zaidi kufanya ushawishi kwa Wabunge waweze kupitisha bajeti mpya ya nchi hiyo iliyopingwa na Wabunge wa Republican wasiotaka sheria ya Bima ya Afya.

Rais wa Marekani Barack Obama akituhubia taifa na kuonesha kusikitishwa na kukwama kupitishwa kwa Bajeti
Rais wa Marekani Barack Obama akituhubia taifa na kuonesha kusikitishwa na kukwama kupitishwa kwa Bajeti
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak amethibitisha kufutwa kwa ziara hiyo ya Rais Obama iliyopangwa kufanyika juma lijalo na sasa Waziri wa Mambo ya Nje John kerry ndiye atamwakilishi Kiongozi huyo.

Serikali ya Marekani imelazimika kufunga kwa mara ya kwanza baadhi ya shughuli zake zisizo na ulazzima mkubwa kutokana na Wabunge wa Chama Cha Republican kukataa kupitisha bajeti ya nchi hiyo wakishinikiza Rais Barack Obama kuachana na sheria ya Bima ya Afya.

Hatua ya kukwama kwa bajeti ya serikali kumetishia kutofanyika kwa shughuli nyingi huku baadhi zikilazimika kufungwa kitu ambacho kimemchukuzi Rais Obama aliyejitokeza na kusisitiza hatoweza kuachana na mpango wake wa sheria mpya ya Bima ya Afya anayoitaja kama mkombozi kwa wananchi.

Uamuzi wa kusitisha shughuli za serikali umekuja kutokana na Mabunge mawili nchini Marekani kushindwa kuafikiana juu ya bajeti mpya ya serikali kutokana na wabunge wa Republican na wale wa Democrats kuwa na misimamo tofauti juu ya suala la sheria ya Bima ya Afya.

Rais Obama amsema hawezi kurudi nyuma kuhusu sheria mpya ya bima ya Afya kama ambavyo Wabunge wa Republican wanavyotaka na badala yake Serikali yake itasamima kidete kuhakikisha bajeti hiyo inapita na hatimaye shughuli kurejee kama zilivyokuwa awali.

Obama amehutubia Taifa na kusema ameshangazwa na hatua ya Wabunge wa Republican kutaka kutumia kisingizo cha Bima ya Afya mfano wa mtu anayetaka kulipwa fedha ili aweze kumuachia mateka anayemshikilia na wao hawatakuwa tayari kuona wananchi wanateseka.

Kiongozi huyo wa Serikali ya Washington amesema wamekamisha kupitisha bajeti mpya kutokana na itikadi yao mbaya inayotaka kuona wananchi wasio na uwezo wa kudumu gharama za matibabu wanaendelea kuteseka wakati serikali yake haitaki kuona wananchi wanapata shida ya matibabu.

Obama amekiri kutokana na kufungwa kwa baadhi ya shughuli za serikali kutokana na kukosekana fedha kumechangia pakubwa athari kwa wafanyakazi na hata wananchi ambao wameshindwa kupata huduma stahiki kwa wakati lakini ameahidi wanapambana kushughulikia hali hiyo.

Wafanyakazi zaidi ya Laki Saba wa Umma nchini Marekani wamelazimika kutoendelea na kazi na watakosa mshahara wao kutokana na serikali kukosa fedha za kugharamia shughuli zake na badala yake watakaopata mishahara ni wanajeshi na wafanyakazi wa sehemu za huduma za afya.

Rais Obama amewaangukia Wabunge wa Congress kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kupitisha bajeti mpya ya serikali ili kuhakikisha shughuli zinarejea na kujiepusha na madhara ya kiuchumi yanayoweza yakachangiwa na kufungwa kwa shughuli hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.