Pata taarifa kuu
KENYA

Wataalamu wa masuala ya kijasusi toka mataifa ya Magharibi na wale wa Kenya waendelea na uchunguzi katika jengo la Westgate

Wataalamu wa masuala ya Kijasusi kutoka mataifa ya Magharibi kwa kushrikiana na wale wa Kenya wanaendelea na uchunguzi wao kwenye jumba la kibiashara la Westgate kubaini iwapo kuna miili zaidi ambayo ilinaswa kwenye vifusi vya jengo hilo. 

Baadhi ya askari wa usalama wa Kenya wakiwa kazini kwenye jengo la Westgate.
Baadhi ya askari wa usalama wa Kenya wakiwa kazini kwenye jengo la Westgate. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku alitangaza kuanza kwa kazi maalumu ya uchunguzi kwa kushirikiana na maofisa toka nchini Marekani,Uingereza na Israel ambao watakuwa na jukumu la kuchunguza madhara yaliyotokana na tukio hilo.

Aidha siku tatu tu baada ya magaidi kuvamia jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi na kusabababisha maafa ya raia 62 na wanajeshi sita wa Kenya, usiku wa jana mtu mmoja alipoteza maisha huku wengine watatu wakijeruhiwa baada ya shambulizi lingine kutokea katika mji wa Wajir Kaskazini mwa Kenya.

Katika hatua nyingine balozi maalumu wa Umoja wa mataifa kwa nchi ya Somalia, Nicholas Kay amekiri kuwa vikosi vya kulinda amani nchini Somalia vinakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu na kwamba ni lazima vikosi hivyo vipatiwe vifaa zaidi ili kupambana na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.