Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Ni Mugabe tena,raisi wa Zimbabwe

Hatimaye tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe imetangaza matokeo ya urais na rais Robert Mugabe kuibuka mshindi kwa asilimia 61.09 akifuatiwa na mpinzani wake waziri mkuu Morgan Tsvangirai,matokeo ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na ulimwengu mzima.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aataendelea na awamu ya saba ya uongozi nchini humo baada ya Tume ya taifa hilo ya uchaguzi kumtangaza mshindi
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aataendelea na awamu ya saba ya uongozi nchini humo baada ya Tume ya taifa hilo ya uchaguzi kumtangaza mshindi REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Awali Waziri mkuu Tsvangirai alilalamikia uchaguzi wa wabunge na uraisi kugubikwa na utata na kuahidi kuchukua hatua za kisheria kupinga matokeo hayo.

Bwana Tsvangirai alidai kuwa chama chake cha MDC hakitakuwa radhi kushirikiana na chama cha raisi Mugabe Zanu-PF.

Vyama hivyo vikuu vya siasa nchini Zimbabwe vimekuwa katika mgogoro tangu mwaka 2009 baada ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo uligubikwa na ghasia.

Matokeo ya mwishoni mwa juma yalionesha chama cha MDC kilibananishwa na kupata ushindi hafifu wa viti vya ubunge 49 wakati chama cha raisi Mugabe Zanu-PF kkikijizolea jumla ya viti 158.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.