Pata taarifa kuu
COLOMBIA-CUBA

Kundi la Waasi la FARC la nchini Colombia limewaua Wanajeshi 19 wa Serikali na Rais Santos ameamuru Jeshi kutositisha kuwashambulia

Jeshi la Colombia limepoteza wanajeshi wake kumi na tisa baada ya kufikwa na umauti kufuatia Kundi la Waasi la FARC kutekeleza shambulizi la kushtukiza kuwalenga kitu ambacho kinatajwa kuzua hofu iwapo mazungumzo baina ya serikali na Kundi hilo yatafanikiwa.

Wapiganaji wa Kundi la Waasi la FARC la nchini Colommbia ambao wanatajwa kuwa kitisho cha usalama
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la FARC la nchini Colommbia ambao wanatajwa kuwa kitisho cha usalama
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili linakuja kipindi hiki Serikali ya Colombia na Kundi la Waasi la FARC wakiwa kwenye mazungumzo ya amani yaliyoanza mwisho mwa mwaka jana yakiwa na lengo la kutaka kumalizwa kwa mashambulizi na mauaji ambayo yamekuwa yakifanywa na Kundi hilo.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amekiri kutoka kwa shambulizi hilo lililochangia vifo vya wanajeshi wake na ametuma salam za rambirambi kwa familia na kuweka bayana wapo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

Santos ameweka wazi wanajeshi hao ni mashujaa kutokana na kupoteza maisha wakiwa kwenye harakati za kulinda nchi yao lakini kwa bahati mbaya wale wasioitakia mema nchi hiyo wameendelea kufanya vitendo vya kihalifu.

Wanajeshi hao walikuwa kwenye doria ya kulinda bomba la mafuta lililopo kwenye mkoa uliopo kwenye mpaka na Taifa la Venezuela ambapo taarifa zinasema waasi wapatao sabini walijitokeza na kuwashambulia kwa risasi.

Rais Santos amesema wanajeshi wengine watano wamejeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo na ametoa amri kwa Vikosi vyake kuendelea kujibu mashambulizi kwa kutumia silaha hadi pale ambapo mgogoro baina yao na Kundi la FARC utakapokuwa umemalizwa.

Kundi la Waasi la FARC limeendelea kufanya masumbulizi yake na hata utekeji nchini Colombia licha ya kukubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na Serikali ambayo yalianza rasmi mwezi Novemba mwaka jana nchini Cuba.

Kundi la FARC linatajwa kuwa na wapiganaji 8,000 ambapo tangu walianzsiha mapoambano dhidi ya Serikali yamechangia vifo vya watu 600,000 huku wengine milioni 3.7 wakiwa hawana makazi na 15,000 hawajulikani walipo.

Mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu kati ya Serikali ya Colombia na Kundi la Waasi la FARC yanatarajiwa kuanza tena tarehe ishirini na nane ya mwezi Julai nchini Cuba katika Jiji la Havana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.