Pata taarifa kuu
SYRIA-ISRAEL

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenye mpaka wa Israel na Syria waongezewa muda

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa miezi sita kwa majeshi ya kulinda amani ya  Umoja wa Mataifa katika eneo la Golan katika mpaka wa Israel na Syria.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi hilo la kulinda amani sasa litamaliza muda wake mwisho wa mwaka huu  na litaongezeka kutoka wanajeshi 900 hadi 1,250.

Eneo la Golan limekuwa uwanja wa mapambano kati ya wanajeshi wa serikali ya rais Bashar Al Assad na waasi katika mgogoro unaoendela kwa mwaka wa pili sasa.

Mark Lyall Grant Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa amesema wanajeshi hao pia watapewa silaha nzito za kujilinda dhidi ya uvamizi kutoka kwa wanajeshi wa Syria au waasi.

Majeshi ya kulinda amani yalitumwa katika eneo mapema miaka ya tisini baada ya baada ya kumalizika kwa vita kati ya Isreal na Syria kuhakikisha amani inadumu katika mpaka wa mataifa hayo mawili.

Kwingineko nchini Syria, Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa miili ya watu 16 ya watu walioteswa na majeshi ya serikali imewasilishwa kwa jamaa zao siku ya Ijumaa.

Mashirika hayo yanasema kuwa maelfu ya watu bado wanazuiliwa na kuteswa na jeshi la rais Bashar Assad baada ya kukamatwa katika maandamano ya kuiangusha serikali ya Assad.

Takwimu za hivi karibu kutoka kwa umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa zaidi ya watu laki moja wameuliwa nchini Syria katika mapigano kati ya wapinzani na wanajeshi wa serikali kipindi hiki ambacho mataifa ya Magharibi yakipanga kuwapa silaha waasi huku serikali nayo ikipata usaidizi kutoka kwa Iran na kundi la Hezbollah kutoka Lebanon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.