Pata taarifa kuu
IMF-ULAYA

Mkuu wa IMF Christine Lagarde ahojiwa kuhusu tuhuma za ufisadi

Viongozi wa Mashtaka nchini Ufaransa wamemhoji Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde kwa tuhuma za ufisadi alipokuwa waziri wa fedha nchini humo.

Mkuu wa taasisi ya fedha kimataifa,IMF Christine Lagarde anakabiliwa na tuhuma za ufisadi
Mkuu wa taasisi ya fedha kimataifa,IMF Christine Lagarde anakabiliwa na tuhuma za ufisadi
Matangazo ya kibiashara

Lagarde aliwasili mahakamani jijini Paris kujibu maswali kutoka kwa viongozi wa mashataka ambao wanatathmini ikiwa afunguliwe mashataka na wizara ya fedha kuhusika na malipo ya Yuro milioni mia tano kumi na tano kwa tajiri Bernard Tapie mwaka 2007.

Lagarde amefika mahakamani siku moja baada ya kutajwa kuwa mwanamke wa saba duniani mwenye nguvu na ushawishi zaidi.

Waziri wa fedha nchini humo Pierre Moscovici amesema kuwa amezungumza na Lagarde ambaye amemhakikishia kuwa anaviamini vyombo vya sheria nchini humo na haki itatendeka.

Hata hivyo msemaji wa serikali Najatt Belkacem anasema siku za Lagarde kusalia kama mkurugenzi mkuu wa IMF huenda zitafikia mwisho ikiwa viongozi hao wa mashataka watampata na kesi ya kujibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.