Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-UMOJA WA MATAIFA

Umoja wa Mataifa UN na Marekani zapinga taarifa za Waasi na Wapinzani kutumia silaha za kemikali iliyotolewa na Wachunguzi wa UN

Timu ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa UN imekanusha haina ushahidi unoanonesha Waasi na Wapinzani nchini Syria wanatumia silaha za kemikali aina ya sarin kama ambavyo imeelezwa jana na Mjumbe wa Kamati ya Uchunguzi Carla Del Ponte.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa UN imekanusha vikali uwepo wa ushahidi unaoonesha Wapiganaji wa Waasi na wale wa Upinzani wamekuwa wakitumia silaha hizo za kemikali kwenye mapambano yao dhidi ya Jeshi la Serikali.

Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa nchini Syria imsema haijafikia suluhisho na kubaini upande gani kwenye mgogoro wa Syria unatumia silaha hizo za kemikali kutokana na kutopatikana kwa ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.

Marekani nayo imekuwa nchi ya kwanza kukanusha uwepo wa matumizi ya silaha za kemikali kwa wapinzani nchini Syria kwani yenyewe awali ilitoa taarifa iliyoonesha Jeshi la Rais Bashar Al Assad ndilo linatumia silaha za kemikali.

Marekani, Uingereza na Israeli zilikuwa nchi za kwanza kutoa ushahidi ya kwamba serikali ya Rais Assad ndiyo inatumia silaha za kemikali katika kuashambulia wapiganaji wa Upinzani licha ya serikali yenye kukanusha hilo.

Msimamo wa Marekani umetangazwa na Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney ambaye ameendelea kushikilia msimamo ule ule ya kuwa Jeshi la Serikali ndilo linatumia silaha za kemikali na si Wapiganaji wa Waasi na wale wa Upinzani.

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO yenyewe imekuwa na msimamo tofauti na kueleza lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli badala ya kukanusha bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.

Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema kuna uwezekano pande zote zinazishiriki kwenye mapambano hayo zikawa zinatumia silaha za kemikali ili kuhakikisha wanshinda vita hivyo.

Rasmussen amezitaka nchi kutokuwa na papara kukanusha tu hizo taarifa kwa sababu wamekuwa wakishirikiana na Wapinzani na badala yake uchunguzi makini ufanyike ili ukweli wa mambo ubainike.

Tayari Baraza la Taifa la Upinzani Nchini Syria SNC limekuwa mstari wa mbele kukanusha wao wanatumia silaha za kemikali wakielekeza kidole cha lawama kwa serikali wakisema ndiyo yenye uwezo huo.

Mapema jumatatu Carla Del Ponte akifanya mahojiano na kituo kimoja cha Utangazaji nchini Uswiss alisema wamepata ushahidi wa awali kulingana na madaktari waliofanya uchunguzi kwa waathirika na kubaini Waasi na Wapinzani ndiyo wanatumia silaha za kemikali zenye sumu ya sarin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.