Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yatishia kuivamia Marekani na Korea Kusini

Korea kaskazini imetoa vitisho vipya vya kupigana vita vya Nuklia baada ya Kuwekwa kwa vikwazo vipya na Baraza la usalama la umoja wa mataifa UNSC dhidi yake. Vitisho vimetolewa na Korea Kaskazini vinalenga kuishambulia Marekani na Korea kusini.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo la Pyongyang limekuja saa kadhaa baada ya Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuongezea makali ya vikwazo kwa Korea Kaskazini baada ya jaribio lake la Nyuklia la tarehe 12 mwezi Februari.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney amesema kuwa Marekani haiogopi na vitisho vya Korea kaskazini kwa kuwa ina uwezo wa kujilinda.

Maazimio yaliyofikiwa na nchi wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa yaliweka vikwazo zaidi vya kuibana sekta ya kibiashara ya Korea kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.