Pata taarifa kuu
Mali-UFARANSA-COTE D'IVOIRE

Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS yakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini Mali

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi ECOWAS inafanya kikao cha dharura jijini Abdijan nchini Cote d'Ivoire leo jumamosi kujadili hali inavyoendelea nchini Mali. Kikao hicho kinafanyika chini ya Mwenyekiti wa ECOWAS Allasane Outtara ambaye pia ni Rais wa Cote d'Ivoire.

Reuters/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje ya Ufaransa Laurent Fabius ni miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria kikao hicho jijini Abdijan.

Jana ijumaa vikosi vya kijeshi vya Mali vikishirikiana na Ufaransa ziliendeleza makabiliano na kufanikiwa kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa unamilikiwa na wapiganaji wa kiislamu walioshikilia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo toka mwaka jana.

Jeshi la Mali na Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa kwa pamoja wamethibitisha kufanikiwa kuudhibiti mji huo uliopo umbali wa kilometa mia saba kutoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.

Hofu ya ukiukwaji wa haki za binadamu imezidi kutanda wakati ambapo maelfu ya raia wanazidi kuyakimbia makazi yao wakihofia mapigano yanayoendelea.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.