Pata taarifa kuu
UFARANSA

Majaji nchini Ufaransa wamhoji rais wa zamani Nicolas Sarkozy

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amefikishwa mahakani na kusomewa mashtaka ya matumizi ya fedha zisizo halali katika kampeni za kuwania urais wa nchi hiyo mwaka 2007. 

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy,
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Sarkozy ambaye amepoteza kinga ya kushtakiwa baada ya kuondoka madarakani mwezi mei na kiti chake kurithiwa na rais wa sasa Francois Hollande anakabiliwa na mashtaka dhidi ya matumizi ya fedha zisizo halali katika kampeni zake za urais wa mwaka 2007.

Sarkozy amefikishwa mahakamani akituhumiwa kupokea jumla ya euro laki moja na elfu hamsini 150,000 toka kwa mwanamke tajiri Liliane Bettencourt na kuzitumia katika kampeni zake.

Sambamba na hayo Sarkozy pia alikiuka sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo kikomo cha matumizi ni euro 4600 pekee.

Rais huyo wa zamani aliwasili sambamba na mwanasheria wake Jean-Michel Gentil huku vyombo vya usalama vikiimarisha ulinzi.

Sarkozy amekanusha kuhusika na rushwa ya aina yoyote ile, hata hivyo kama atakutwa na mashtaka atakabiliwa na adhabu kama ilivyokuwa kwa Rais aliyemtangulia Jacques Chirac ambaye alihukumiwa kifungo alipotoka madarakani mwaka 2007 baada ya kukutwa na hatia ya kutokuwa mwaminifu na ubadhirifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.