Pata taarifa kuu
Cambodia

Mfalme wa Cambodia afariki dunia

Mfalme wa zamani wa Cambodia Norodom Sihanouk amefariki dunia nchini China akiwa na umri wa miaka 89, kutokana na maradhi ya mshtuko wa moyo muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

REUTERS/Samrang Pring
Matangazo ya kibiashara

Mwanae mfalme Norodom Sihamoni na waziri mkuu Hun Sen wameondoka Phnom Penh mchana kuelekea jijini Pekin wakiwa na huzuni kubwa.

Mwili wa marehemu mfalme Norodom utasarifishwa siku jumatano hadi nchini Cambodia ambapo shughuli za maomblezo zitakwenda hadi Octoba 23 na baadae mwili wake utawekwa kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wananchi wa Cambodia kwa ajili ya shughuli za kumuaga.

Mfalme huyo wa zamani alikuwa anaeshi jijini Pekin tangu kupindi kadhaa ambako alilazimika kusalia nchini humo kwa ajili ya matibabu ambapo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari, saratani, na shinikizo la damu.

Mfalme Sihanouk ni mmoja kati ya viongozi wa kifalme waliotawala kwa muda mrefu barani Asia, alitowa madaraka kwa mwanae Sihamoni mwaka 2004, ambae amesema kwamba mfalme Sihanouk hakuwa wa familia bali alikuwa ni mfalme wa wananchi wa taifa la Cambodia na historia.

Serikali ya pekin imesema kusikitishwa na kifo hicho cha mtu walioumuita rafiki mkubwa, huku mataifa mengine barani Asia yakiendelea kupeleka salam za rambirambi.

Kiongozi huyo aliowa mara sita katika uhai wake, na mke wake wa mwisho Monique Izzi aliewahikuwa mwanamitindo mwenye aisli ya Italia na kufaanikiwa kuzaa watoto kumi na wanne ambapo watano waliuawa katika utawala wa Khmers Rouges chini ya uongozi wa Pol Pot.

Mnamo siku za nyuma alikuwa akiwafahamisha wapenzi wake kuhusu afya yake na maswala ya siasa kupitia mtandao wake wa Internet, Octoba 2009 alifahamisha kwamba sasa ameishi miaka mingi, na kwamba imekuwa mzigo mkubwa sana kwake.

Miaka miwili baadae wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu kutoka uhamishoni, aliahidi umati uliokuwa kwenye sherehe kwamba hatorudi tena ugenini, lakini Januari 2012 aliondoka Phom Penh na kuelekea China kwa sababu za matibabu.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.