Pata taarifa kuu
DRC-Francophonie

Mkutano wa nchi zinazungumza Kifaransa, Francophonie waanza nchini DRC

Viongozi wa nchi wanachama zinazozungumza lugha ya Kifaransa leo Ijumaa wameanza mkutano wao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo pamoja na viongozi wengine mkutano huo unahudhuriwa na Rais wa Ufaransa Francois Hollande.

REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unahudhuriwa viongozi wa mataifa 75 yanayozungumza lugha ya Kifaransa chini ya uenyeji wa Rais wa DRC Joseph Kabila ambaye pia atachukua nafasi ya uenyekiti wa Francophonie kwa kipindi cha miaka miaka miwili ijayo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameanzia ziara yake ya kwanza Barani Afrika nchini Senegal ambako amekutana na Rais wa nchi hiyo Macky Sall kabla ya kuelekea nchini DRC.

Akiwa nchini Senegal masuala yaliyopewa kipaumbele ni pamoja mgogoro wa nchi ya Mali kupelekewa jeshi la ECOWAS ambalo Ufaransa imesema italisaidia kama hakutakuwa makubaliano baina ya Serikali na waasi kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakati huohuo Maelfu ya watu wameandamana mjini Bamako, nchini Mali kutoa wito wa kufanyika uvamizi wa kijeshi kutoka majeshi ya jumuia ya kiuchumi ya nchi za magharibi, ECOWAS kusaidia kupambana na makundi ya kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Maandamano hayo yamefanyika wakati Ufaransa na washirika wengine wa umoja wa Mataifa wakiishinikiza ECOWAS na Umoja wa Afrika kutoa mapendekezo ndani ya siku 30 juu ya namna ya kushughulikia tatizo la Kaskazini mwa Mali.
Waandamanaji wamemtaka Kepteni Amadou Haya Sanogo na vikosi vingine kuongoza mapambano hayo.
Sanogo aliongoza mapinduzi ya tarehe 22 mwezi March na kumuangusha Rais wa taifa hilo, Amadou toumani Toure na kusababisha hali ya vurumai hali iliyotoa mwanya kwa makundi ya kiislamu na kudhibiti na kuweka Sharia katika eneo la kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.