Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-POLOKWANE

Julius Malema ashtakiwa kwa makosa ya kufanya biashara haramu ya fedha

Mahakama ya Polokwane iliyoko mjini Limpompo nchini Afrika Kusini imemshtaki kiongozi wa zamani wa vijana wa chama cha ANC Julius Malema kwa makosa ya kushiriki biashara haramu ya fedha na kufanya mikataba isiyo halali.

Julius Malema akiwa mahakamani siku ya Jumatano
Julius Malema akiwa mahakamani siku ya Jumatano REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Malema na wenzake wamepandishwa kizimbani hii leo ambapo wote kwa pamoja wamekana kuhusika na mashtaka dhidi yao na mahakama imewaachilia huru kwa dhamana.

Kesi yao imepangwa kusikilizwa tena tarehe 28 ya mwezi November mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utakuwa ukiwasilisha ushahidi wake dhidi ya Malema.

Ulinzi mkali umewekwa nje ya mahakama hiyo ukiwemo uzio maalumu kuingia eneo la mahakama hiyo ambapo kiongozi huyo anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya uchochezo na rushwa yanayomkabili.

Tayari kiongozi huyo yuko ndani ya mahakama ya Polokwane akisubiri kusomewa mashtaka yake ikiwemo kuamuliwa iwapo ana kesi ya kujibu ama la kuhusiana na kesi ambayo imewasilishwa dhidi yake.

Kabla ya kuingia mahakamani hapo Malema alijisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha Polisi ambacho alikuwa anatakiwa kufika na kisha kuwekwa kizuizini kabla ya kupelekwa mahakamani.

Maelfu ya wafuasi wake wamekusanyika nje ya mahakama hiyo wakiwa na mabango mbalimbali wakidai kesi dhidi ya kiongozi wao ni zakisiasa zaidi na zinalenga kumchafua kiongozi wao.

Malema anatuhumiwa kutumia fedha za chama vibaya wakati akiwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha ANC pamoja na tuhuma za kudaiwa kukwepa kodi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.